"Kwa
sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya
awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi, nyumba za
watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi
mapya, " alisema.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) katika mikutano ya
hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua, wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Alikuwa
akijibu maombi ya wabunge wa majimbo ya Ulyankulu na Kaliua ambao walisema kuna
haja ya kuigawa wilaya ya Kaliua ili kusogeza huduma kwa wananchi waishio
kwenye kata zilizo mbali na tarafa.
Akizungumzia
kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Waziri Mkuu alisema
Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha
zoezi hilo itatoa taarifa.
Ili
kuharakisha zoezi hilo, Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi
pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi
wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.
"Tumeamua
kuweka beacons katika maeneo yote ya hifadhi ili kubaini mipaka imepita
wapi. Wananchi mkiwaona watu wa hifadhi wanapita huko msigombane nao. Ni
hatua ya awali ya kubaini maeneo ya mipaka. "
"Niwasihi
wanavijiji wote, vijiji vilivyomo kwenye hifadhi visiendelee kupanua maeneo
yake. Mbaki hivyo hivyo hadi Serikali itakapoamua vinginevyo, "
alisema.
Alisema
zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi likikamilika na taarifa kutolewa,
Serikali itatoa uamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya
Hifadhi.
Akiwa
Kaliua, Waziri Mkuu alielezwa na Mbunge wa jimbo hilo, Mheshimiwa Magdalena
Sakaya kuwa wananchi wanashindwa kujenga makazi ya kudumu katika maeneo
waliyopo kwa sababu wanatishiwa kwamba wapo hifadhini.
Waziri
Mkuu alisema Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho
ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya
Wakimbizi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, AGOSTI 12, 2017.
No comments:
Post a Comment