MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLESENDEKA AKIZUNGUMZA NA WAFANYA KAZI WA KAMPUNI HIYO AMBAO WAMEMPATIA KERO MBALIMBALI
KWA MACHUNGU MAKUBWA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA TANWAT WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA KWA MAKINI NA KUSEMA HAWAJALIPWA MISHARA YAO KWA ZAIDI YA MIEZI MINNE.
HAPA MKUU WA MKOA AMEWAKALIA KOONI VIONGOZI WA KAMPUNI YA TANWAT KWAMBA HAWAJAPELEKA MICHANGO YA WAFANYAKAZI KWA MUDA MREFU HADI SASA WAMEPELEKA MICHANGO MARA MBILI TU KINYUME NA SHERIA.
MKURUGENZI WA KAMPUNI DKT RAJEEV AKIJITETEA MBELE YA MKUU WA MKOA HUYO
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLESENDEKA AKIMSISITIZA DKT RAJEEV JUU YA KUTENDA HAKI KWA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLESENDEKA BAADA YA KUWASILI KWENYE KIWANDA HICHO MKURUGENZI WA KAMPUNI YA TANWAT DKT RAJEEV AKAINGIA KWENYE GARI KWA LENGO LA KUKIMBIA ASIONANE NA MKUU WA MKOA LAKINI WAFANYAKAZI WAKASHIKIA KIDEDEA KWA KUFUNGA GETI ILI AKUTANE NA MKUU HUYO WA MKOA NDIPO MAZUNGUMZO YAKAANZA NJE YA MASHINE LAKINI NI NDANI YA FENZI ZA KIWANDA HICHO.
NJOMBE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopha Olesendeka ameahidi kuunda tume kwaajili ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Tanwat ikiwemo ya kuwepo kwa mikataba miwili tofauti ya malipo ya mishahara kinyume na sheria.
Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya Tanwat Mkuu wa Mkoa Olesendeka ametaka utawala kuheshimu mikataba yao haiwezekana wajili kuweka mikataba miwili yaani mkataba ulioelekezwa na serikali na mkataba unaolipa mishahara tofauti na wa serikali.
Olesendeka ameyasema hayo baada ya kuwasikiliza wafanyakazi wa kiwanda cha Tanwat na kupokea kero mbalimbali ikiwemo za kucheleweshwa kwa mishahara,kutopewa haki za likizo za uzazi, kuumia kazini na kushindwa kupeleka michango ya wafanyakazi.
Olesendeka amewataka viongozi na wafanya kazi kuacha ubaguzi wa rangi wakati wa kuajili wafanyakazi huku wafanyakazi nao wakitakiwa kuondoa mawazo ya ukabila katika kuomba ajili nakwamba kila mmoja anatakiwa kuheshimu mamlaka,sheria na taratibu bila kujali cheo chake.
"Kampuni hii ipo kwa mujibu wa sheria bodi yao wamemwajili Rajeev, wamemwajiri na mwingine ila tunachotaka ni kuwafanya waliopo hapa na wao waheshimu mamlaka ,waheshimu watu,waheshimu taratibu, waheshimu sheria ,mtu ambaye hataheshimu ataondoka kwa ubaya wake na hapa hatutajali huyo ni nani" Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Olesendeka amesema sheria ya Fidia ya wafanyakazi kipindi cha nyume ilikuwa haijakaa vizuri kwa sababu ilikuwa ya mwaka 1947 lakini imekuja ya mwaka 2008 ilianza kuweka utaratibu wa fidia ambao unafanana kidogo na hali ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi waliopo kwa wakati huu
"Yeyote angepata ulemavu wa kudumu zingeletwa Ndege ziwachukue mpelekwe Apolo India au Nairobi ili akatibiwe lakini wafanyakazi wameumia mmeshindwa kuwasaidia waliopata ulemavu wa kudumu nasema kwenye mfuko huu wa kisheria mmechangia miezi miwili tu tangu muanze na ulipaswa kulipa kwa miezi yote na sheria inakutaka wewe uliyeshindwa kulipa ufungwe miaka miwili jela na ukitoka ulipe fedha zote za wafanyakazi" Aliyasema Olesendeka.
Olesendeka amemtaka mkurugenzi wa kampuni hiyo kutafuta mtu wa kumsaidia katika kumaliza matatizo yanayowakabili wafanyakazi na anayeweza kuzungumza na wafanyakazi akaeleweka na kusema anatarajia tume yake itakwenda kufanya uchunguzi kwa kiina na kupata tatizo lililopo na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kwani kuna walemavu walioiupata wakiwa kazini wengine hawana mikono lakini hawajasaidiwa chochote na kampuni hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa ametaka pia wafanya kazi kuacha tabia ya kutoroka na kufanya udanganyifu katika kazi badala yake wawe waaminifu katika kazi ili kazi ifanyike na kupata maendeleo kwaajili yao na taifa.
Kwa Upande wake wafanyakazi wa kampuni ya Tanwat wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa huyo wamesema wamekuwa wakidhalilishwa,kunyanyaswa na kutolipwa fidia wakati wakitumia fedha zao kwenye matibabu kwa tatizo alilopata akiwa kazini.
Edmond Munubi ni afisa tawala ambaye kwa taaluma ni Mhasibu amekili kupokea baadhi ya malalamiko ya wafanya kazi kuhusiana na changamoto zinazowakabili huku malalamiko mengine ya wafanyakazi hao akisema siyo ya kweli.
No comments:
Post a Comment