Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, January 12, 2017

DIWANI WA KATA YA RAMADHANI AENDELEA NA ZIARA KATANI KWAKE

 DIWANI KATA YA RAMADHANI GEOGE SANGA AKIWA KWENYE OFISI YA SHULE YA MSINGI ITULIKE
 AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA  DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHANDEMA KATA BWANA BASHIR


 HAPA DIWANI YPO KWENYE MKUTANO NA WANANCHI WA MTAA WA ITULIKE NJOMBE MJINI
 MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA ITULIKE AKIZUNGUMZA KWA KUMKARIBISHA DIWANI
 DIWANI WA KATA YA RAMADHANI GEOGE SANGA AKIONGEA NA WANANCHI WA MTAA WA ITULIKE



NJOMBE

Diwani wa kata ya Ramadhani Geoge Sanga amehimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Afya wa taifa wa Bima ya Afya kwaajili ya kupatiwa matibabu bure kwa mwaka mzima na kutaka kuondoa imani ya kwamba dawa hazipo hospitalini.

Sanga amesema tatizo la kukosekana kwa dawa wananchi wanatakiwa kupeleka malalamiko baada ya kujiunga na kukosa huduma za dawa kuliko ilivyo sasa wananchi wanakataa kujiunga kwa madai dawa hakuna ikiwa hawajajiridhisha kama dawa zitakuwa hazipo.

Amesema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wachache ambao wakiugua wanakosa hela ya kununulia dawa pindi wanapokuwa wameugua jambo ambalo limemulazimu kuhimiza kujiunga kwneye mfuko huo kwa manufaa yao .

Katika hatua nyingine Diwani huyo Sanga amewataka wananchi kuukataa umasikini kwa kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya kuinua uchumi wao binafsi na kwa serikali kwa ujumla na kutaka kuwabeza baadhi yao wanaopinga maendeleo yao.

Amesema kufanya kazi ni jambo lisilopingika kwa kila mwananchi kwani ni moja ya kukuza uchumi na kuongeza chakula ambapo serikali inaendelea kufungamana  na wananchi katika kuhimiza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wa kilimo cha Parachichi diwani huyo anasema Wanachi wa kata ya Ramadhani wametakiwa kujikita katika kilimo cha Parachichi na ufugaji kuku kwa manufaa yao ili kukuza sekta ya uchumi na kukuza pato la halmashauri.

Wito  huo  umetolewa na Diwani wa kata ya Ramadhani Geoge Sanga wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Itulike kuhusiana na maendeleo ya kata na mitaa iliyopo ambapo amesema umasikini unatakiwa kukemewa na kila mmoja.

Mwalimu Sanga amesema wakulima wa Zao la Parachichi wanatakiwa kuwashirikisha watalaamu wa kilimo katika kuboresha kilimo cha parachichi huku akipongeza wakulima wa Itulike kwa kupokea vizuri mradi wa kilimo cha parachichi.

Aidha Sanga amewaagiza maafisa kilimo na mifugo kuhakikisha wanawatembelea wafugaji na wakulima katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo ili kutoa ushauri juu ya kilimo cha  mazao mbalimbali huku wafugaji nao wakiwatumia maafisa mifugo kuboresha miradi ya ufugaji.

Wananchi wa mtaa wa Itulike wamepongeza kwa elimu na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa watalaamu mbalimbali lakini wameomba kutafutiwa soko la matunda hayo watakapoanza kuvuna.

.....................................................................

No comments:

Post a Comment