Afisa
Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge
(aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof
Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa
pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea
Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara
baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na
Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo. Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa
akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo
alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia
Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw.
Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani)
alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri. Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Bi. Nikusubila Maiko (wa kwanza kulia) akiwa katika mkutano
huo. Kutoka kushoto ni Meneja Ufundi wa NIDC, Kironde Kaijage pamoja na
Katibu wa Waziri Prof. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano huo.
SERIKALI
imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi
vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia
Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo
na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya
ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu
za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL.
Mheshimwa
Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo
mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na
kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na
kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo
ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.
'Natoa
agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga
Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya
juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika
majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa
tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo
hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.'
Akiwa
katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka
Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu
ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na
kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.
Mkuu wa Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC),
Abdul Mombokaleo (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa (kushoto) alipotembelea
kukagua utendaji kazi wa kituo hicho.
'TTCL
mna deni kubwa kwa Wananchi. Tumeondoa vikwazo vingi vilivyokuwa
vikiwakwamisha na sasa tunataka kuona kasi ya uhakika ya utendaji kazi.
Tumewalipa Bharti Airtel na kuvunja ubia nao, tumewafutia madeni,
tumewakabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha Kimataifa cha
kuhifadhia kumbukumbu mviendeshe kwa niaba ya Serikali.
Yote
haya yamefanyika kwa nia moja ya kuwajengea uwezo ili mtimize majukumu
yenu vizuri.' amesema Waziri Mbarawa.
Katika hatua nyingine, Waziri Profesa Mbarawa amepongeza jitihada kubwa
zinazofanywa na TTCL katika kuboresha huduma zake nchini. Aidha, Mhe
Mbarawa ameeleza kuridhika kwake na kasi kubwa ya kusambaza huduma za
mtandao wa 4G LTE na kujitangaza zinazofanywa na Kampuni hiyo katika
maeneo mbali mbali nchini.
Awali
katika taarifa yake fupi kwa Mhe Waziri, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL Bw Waziri Kindamba amesema, hadi kufikia Januari 16, 2017 Mikoa 7
ya Tanzania bara inapata huduma kwa teknolojia ya 4G LTE ambayo ni Dar
es Salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro,Mwanza, Mbeya na Arusha. Tarehe 11
Januari 2017, siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar, TTCL ilizindua huduma za 4G LTE mjini Unguja.
Bw
Kindamba ameongeza kuwa, kutokana uhusiano wa shughuli za kiuchumi na
kijamii baina ya Visiwa vya Unguja na Pemba, TTCL inakusudia kupeleka
huduma za 4G LTE Kisiwani Pemba katika muda mfupi ujao ili kulifanya
eneo lote la Tanzania Visiwani kufikiwa na huduma na kusaidia katika
ukuaji wa shughuli za kiuchumi,huduma za kijamii,ulinzi na usalama
katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment