Na Mwandishi wetu
Bondia nyota wa ngumi za
kulipwa nchini, Cosmass Cheka Jumamosi June 4 anapanda jukwaani kwenye
uwaja wa Ndani wa Taifa kupambana na bondia wa Malawi, Chrispin Moliyati
katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa Universal Boxing Union
(UBO) wa uzito wa Super feather.
Pambano hilo la raundi 12
limeandaliwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Advanced Security,
Juma Ndambile kwa lengo la kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Ndambile ambaye ni meneja wa
Cheka alisema kuwa ameaua kumtuafutia mpinzani wa nje bondia wake kwa
lengo la kumpandisha kiwango ili aweze kucheza mapambano makubwa
duniani.
Alisema kuwa ameamua kuondokana
na kuwaandalia mabondia wake mapambano dhidi ya mabondia wa hapa hapa
kwani hawapati uzoefu wa kimataifa.
Kwa upande wake, Cheka alisema
kuwa amejiandaa vyema kwa pambano hilo na anataka kuonyesh ubora wake
katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Cheka alisema kuwa anatarajia kushinda katika pambano hilo ili kuendeleza rekodi yake katika ngumi za kulipwa.
“Moliyati ni bondia mzuri na
najua atanipa upinzani mkali, lakini sitakubali kupoteza katika ardhi ya
Tanzania, nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo,” alisema.
Mbali ya mapambano hayo, leo pia kutakuwa na ‘mawe’ ya aina yake katika mapambano ya utangulizi.
Bondia nyota, Japhet Kaseba
atawania ubingwa wa Taifa wa TPBC Limited dhidi ya bondia nyota kutoka
Zanzibar, Amour Mzungu katika pambano la uzito wa juu, Pia Alphonce
Mchumiatumbo atazipiga na bondia Mussa Ajibu kutoka Malawi katika
pambano la uzito wa juu kabla ya Ashraf Suleiman kuonyeshana kazi na
Aliki Gogodo wa Malawi katika pambano la uzito wa juu pia.
Pambano lingine la ubingwa
litakuwa kati ya bondia Shabani Kaoneka dhidi ya Zumba Kukwe la uzito wa
middle raundi 10 ambapo Yonas Segu atazichapa na bondia wa Malawi,
Wilson Masamba katika pambano la uzito wa Light-Welter la raundi nane.
Mabondia wa kike, LuluKayage atazichapa na Enelesi Nkwanthi katika pambano la uzito wa bantam la raundi sita.
No comments:
Post a Comment