AFISA MASOKO WA KAMPUNI YA ASASI LIPITA MTIMILA BAADA YA KUPOKEA NGAO YA USHINDI WA USINDIKAJI MAZIWA
WADAU WA ASASI WAKIWA NA AFISA MASOKO WA KAMPUNI YA ASAS KWENYE MAADHIMISHO YA UHAMASISHAJI UNYWAJI MAZIWA ILIYOFANYIKIA NJOMBE KITAIFA
MGENI RASMI MARY MASHINGO AKIWA NA KAIMU MKUU WA MKOA WA NJOMBE ANATORY CHOYA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA LUDEWA
WANAFUNZI MBALIMBALI WAKIWA KWENYE MAANDAMANO KUELEKEA UWANJA WA MAONESHO WA MPECHI
MGENI RASMI HAPA ANATOA HOTUBA YAKE KWA WAKAZI WA NJOMBE NA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
WEMA NGIMBUDZI AMBAYE AMEPATA NG'OMBE WA MAZIWA SIKU HIYO YA MAADHIMISHO YA UHAMASISHAJI UNYWAJI MAZIWA KITAIFA YALIYOFANYIKIA NJOMBE
WANANFUNZI MBALIMBALI WAKIELEKEA KUPELWA MAZIWA NA MGENI RASMI
HAPA WADAU MBALIMBALI WANAPEWA VYETI VYA WASHINDI MBALIMBALI
LIPITA MTIMILA WA ASAS AKIPOKEA CHETI CHA USHIRIKI KWA MGENI RASMI
TANGA FRESH NAO WAMEPOKEA CHETI CHA USHIRIKI
NJOMBE MILK FACTORY MUWAKILISHI WAO ANAPOKEA CHETI KWA MGENI RASMI
MSHINDI WA KWANZA KWA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA ASAS AKIWAKILISHWA NA AFISA MASOKO WAO LIPITA MTIMILA ANAPOKEA NGAO YA USHINDI
Serikali Imejikita Kuboresha Huduma Ya Uhimilishaji Na Tayari Ina Vituo Vya Kutosha Kwa Sasa Ambavyo Vinaweza Kusambaza Mbegu Na Kimiminika Kwaajili Ya Kuhifadhia Mbegu Hizo Ili Kuongeza Idadi Ya Mifugo Huku Ikiwahamasisha Wananchi Kujiunga Kwenye Vikundi Katika Ushirika Kwaajili Ya Kuwasaidia Na Kuwawezesha Kisheria Kupatiwa Mitaji Ya Kuwezesha Kwenye Tasnia Ya Maziwa.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Katibu Mkuu Wizara Ya Mifugo , Kilimo Na Uvuvi Dakt Mary Mashingo Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Maziwa Ambayo Yamefanyikia Mkoa Wa Njombe Kitaifa Yenye Ujumbe Usemao Jenga Tabia Ya Kunywa Mziwa Kwa Afya Na Uchumi.
Aidha Dkt Mashingo Amsema Endapo Wafugaji Watajiunga Kwenye Vikundi Wataweza Kutatua Matatizo Yatakayojitokeza Na Kusema Kuwa Tatizo Kubwa Linalowakabili Wakulima Na Wafugaji Ni Kukosekana Kwa Mitaji Ambapo Serikali Inahamasisha Taasisi Za Kifedha Kusaidia Kutoa Mikopo Ili Wafugaji Hao Wapate Mitaji Ya Kuwekeza Kwenye Sekta Ya Maziwa Huku Serikali Ikipigania Kufufua Viwanda Ambavyo Vilikuwa Havifanyi Kazi.
Akisoma Taarifa Fupi Mbele Ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti Wa Baraza La Maziwa Nchini Ally Magani Amesema Maadhimisho Hayo Hufanyika Kila Mwaka Hapa Nchini Yakiwa Na Lengo La Kuhamasisha Wananchi Kunywa Maziwa Salaama Kwaajili Ya Afya Na Uchumi Pamoja Na Ufugaji Wa Ng'ombe Wa Maziwa Zaidi.
Katika Kuadhimisha Maadhimisho Ya Uhamasishaji Wa Unywaji Maziwa Kitaifa Yamefanyika Mkoa Wa Njombe Huku Mgeni Rasmi Huyo Akikabidhi Zawadi Kwa Washindi Na Washiriki Mbalimbali Wa Sherehe Hizo Akiwemo Mlemavu Wa Macho Wema Ngimbudzi Ambaye Amepewa Ng'ombe Mmoja Wa Maziwa Na Kampuni Ya Asas Iliyopewa Ngao Ya Ushindi Wa Uzarishaji Wa Maziwa .
No comments:
Post a Comment