Saturday, May 21, 2016
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN AKABIDHI VIFAA VYA KUWAWEZESHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO KUSOMA VIZURI KATIKA SHULE YA MSINGI KIBENA MJINI NJOMBE
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN VICKY NTETEMA AKIWASALIMIA WATOTO HAO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO WALIOKO SHULE YA MSINGI KIBENA MJINI NJOMBE
KAIM MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIBENA AMBAKO WATOTO WENYE ULEMAVU WANASOMA
KUSHOTO NI KAIM MKURUGENZI WA KAMPUNI YA TANWAT DKT RAJEEV SINGH AKIWA NA AFISA UTAWALA WA KAMPUNI HIYO EDMUND MUNUBI
WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WAKIWA WAMEFRAHI KUPEWA ZAWADI NA KUFIKIWA NA WAGENI HAO WANAOWASABAHI SHULENI NA KUWAPATIA MOYO WATOTO HAO
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN VICKY NTETEMA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA MSINGI KIBENA PAMOJA NA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO
BABU KONDO SEIF AKIWAFUNDISHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NAMNA YA KUTUMIA VIFAA VINAVYOSAIDIA KUONA MBALI {VIONA MBALI ILI WAWEZE KUONA VIZURI MAANDISHI WANAPOSOMA
KIFAA HICHO CHA KUKUZA MAANDISHI KWENYE DAFTARI NA HAPA ANAMUELEKEZA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI AWEZE KUONA KWA URAHISI
BABU KONDO SEIF NI AFISA UTETEZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN AKIMUELEKZA PIA MWANAFUNZI MWENYE ULEMAVU WA MACHO KUTUMIA KIFAA CHA KUONA MBALI
HIKI NDICHO KIFAA KILICHOTENGENEZWA NA KAMPUNI YA TANWAT LEADING STEND {MEZA YA KUSOMEA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO KINACHOWASAIDIA WASIINAME SANA NA KUPATA MAUMIVU YA MGONGO.
HAPA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN VICKY NTETEMA AKIKABIDHI VIFAA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI NA MACHO WA SHULE YA MSINGI KIBENA.
HAPA AMEHIMIZA WATOTO HAO KUSOMA KWA BIDII KAMA ALIVYOSOMA BABU KONDO SEIF
Shirika Lisilo la Kiserikali la Under The Same Sun Limetoa Msaada wa Vifaa Vyenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni Tatu Kwa Ajili ya Kusomea Wanafunzi Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) na Macho Kwa Wanafunzi Katika Shule ya Msingi Kibena.
Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Msaada Huo Mkurugenzi wa Shirika Hilo Bi.Vicky Ntetema Amesema Wametoa Msaada Huo Kwa Lengo la Kuwasaidia Kukabiliana na Changamoto Zinazowakabili Wakati wa Kujifunza Shuleni.
Aidha Bi.Ntetema Ameipongeza Kampuni ya TANWATT Mjini Njombe Kwa Kutengeneza Meza Kwa Ajili ya Kusomea Wanafunzi Wenye Ulemavu wa Macho na Ngozi Ambao Wamekuwa Wakikabiliana na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Kuumia Shingoni na Mgongoni Wakati wa Kujifunza Shuleni.
Naye Afisa Utetezi wa Shirika la Under The Same Sun Kondo Seif Ameitaka Jamii Kutowatenga Watu Wenye Ulemavu , Huku Akieleza Kuwa Ulemavu wa Ngozi Unatokana na Ukosefu wa Madini ya Meranini Mwilini Yanayosababisha Kutokuwepo Kwa Rangi Nyeusi Kwenye Ngozi na Nywele Yaani Yenye Vinasaba na Kwamba Tatizo Hilo Lipo Duniani Kote.
Kwa Upande Wake Afisa Elimu Wa Elimu Maalum wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mwalimu Samwel Kingililwe Amelishukuru Shirika la Under The Same Sun Pamoja na Kampuni ya Tanwat Kwa Msaada Waliotoa na Kueleza Kuwa Walemavu Wana Mahitaji Mengi Wanaotakiwa Kusaidiwa Huku Akiyaomba Mashirika , Kampuni na Taasisi Mbalimbali Kuendelea Kuisaidia Serikali Kukabiliana na Matatizo na Changamoto Zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu.
Nao Baadhi ya Wanafunzi Waliopatiwa Msaada Huo Akiwemo Julius Lihwehuli Wamesema Vifaa Hivyo Vitawasaidia Katika Kujifunza Kwao Hasa Katika Kusoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment