Na Rabi Hume, Modewjiblog
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda
ya Mbeya.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni
sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia
wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa,
“Sera
ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na
wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa
gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Mh.Ummy
Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000
ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka
hilo, Cornel Mkeng'e
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya
Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.
No comments:
Post a Comment