MENEJA BENKI YA CRDB MKOA WA NJOMBE ARISON ANDREW AKIZUNGUMZA NA MUWEZESHAJI BWANA NGEREJA MCHARO KUTOKA MAKAO MAKUU YA BENK YA CRDB KABLA YA SEMINA YA SIKU MOJA KUFANYIKA KWA WADAU WA BENKI HIYO NJOMBE
MENEJA BIASHARA WA BENK YA CRDB NJOMBE NASSIB MWENDADI AKISAINISHA MAJINA KWA WANAHISA WANAOINGIA KWENYE SEMINA HIYO
MWEZESHAJI KUTOKA MAKAO MAKUU YA CRDB BENK NGEREJA MCHARO AKITOA AKITOA UFAFANUZI JUU YA UMILKIKI WA HISA KATIKA BENKI
WATEJA WA BENKI YA CRDB NJOMBE NA WANAHISA WAKIWA KWENYE SEMINA HIYO NA HAPA NI MARA BAADA YA KUINGIA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
MENEJA CRDB ARISON ANDREW AKIFUNGUA SEMINA HIYO
MUWEZESHAJI WA SEMINA HIYO KUTOKA MAKAO MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM
NGEREJA MCHARO MWEZESHAJI KUTOKA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB
MENEJA BIASHARA WA BENK YA CRDB NJOMBE NASSIB MWENDADI AKISAINISHA MAJINA KWA WANAHISA WANAOINGIA KWENYE SEMINA HIYO
CLEMENCE MALEKELA AKIWA NA WANACHAMA WENGINE WAKISIKILIZA KWA UMAKINI SEMINA YA CRDB
Benki Ya CRDB Mkoani Njombe Imefanikiwa Kufungua Matawi Mbalimbali Ya Benki Hiyo Katika Halmashauri Zilizopo Mkoani Humo Ikiwemo Wilaya Ya Wanging'ombe,Makete,Wilaya Ya Njombe Na Makambako Ambapo Kwa Sasa Inajiandaa Kwenda Kufungua Tawi Wilaya Ya Ludewa Ili Kurahisisha Utoaji Wa Huduma Za Kifedha Kwa Wateja Wake.
Meneja Wa Benki Ya CRDB Mkoa Wa Njombe Arison Andrew Akiongea Mara Baada Ya Semina Ya Siku Moja Iliyotolewa Kwa Wanahisa Na Wateja Mbalimbali Wa Benki Hiyo Ametaka Wateja Wa Benki Hiyo Kuongeza Jitihada Za Kununua Hisa Na Kufungua Akaunti Ili Waweze Kuwa Wamiliki Wa Benki Hiyo Kwaajili Ya Manufaa Ya Kuinua Uchumi Wao.
Aidha Bwana Andrew Amesema Benk Hiyo Inaendelea Na Jitihada Za Kutoa Elimu Kwa Wananchi Juu Ya Umuhimu Wa Benki Hiyo Na Kwamba Imekuwa Ikitoa Mikopo Kwa Wajasiliamali ,Watumishi Wa Serikali Na Makampuni Ya Watu Binafsi Na Mikopo Ya Makapuni Makubwa Kwa Riba Ambayo Inawezekana Kurejesha Kwa Urahisi.
Kwa Upande Wake Afisa Wa Benki Kutoka Makao Mkuu Ya Benki Ya CRDB Dar Es Salaam Ngereja Mcharo Amesema Kwa Wanahisa Ambao Wanashindwa Namna Ya Kupata Gawio Zao Benki Hiyo Imeanzisha Akaunti Maalumu Inayoitwa Busara Ambayo Mteja Atakuwa Anapata Gawio Moja Kwa Moja Kupitia Akaunti Yake Na Pia Itasaidia Kuwepo Kwa Usalaama Wa Pesa Zao.
Kwa Upande Wake Washishiri Wa Semina Hiyo Wamepongeza Benki Hiyo Ya CRDB Kwa Jitihada Ambazo Zimefanyika Za Kufungua Matawi Mbalimbali Ya Benki Ya CRDB Mkoa Wa Njombe Na Kutaka Wananchi Kujiunga Na Benki Hiyo Kwani Imeweka Utaratibu Mzuri Wa Kumnufaisha Mteja Wake Nakwamba Kwa Sasa Watakwenda Kununua Hisa Kwa Wingi Ili Wamiliki Benki Hiyo Na Kupongeza Kwa Kuanzisha Akaunti Ya Busara.
No comments:
Post a Comment