Mtaalam
wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester
Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo,
Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango
iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma
ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam
wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester
Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo,
Itirima.
---
Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu.
Wananchi
wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za
kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi
wengi.
Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki
iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes
Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio
vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo
linalowafanya kuendea kuwa maskini.
"Nawaasa
wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka
mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu
anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa
kuwahudumia," alisema Meena.
Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza
kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango.
Akiongea
mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa
muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa
mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya
watu.
No comments:
Post a Comment