Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, April 28, 2016

RC.MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA WAMILIKI WA BENDI KUPELELEKA MAPENDEKEZO MAPYA SHERIA YA KUFANYA BIASHARA HIYO.

Sehemu ya wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika ukumbi wa Vijana leo kuwasilikiliza juu ya kilio wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki juu ya agizo la kufunga kumbi hizo saa sita leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WADAU wa Muziki na wamiliki wa bendi wamekutana kwa ajili kuangalia jinsi ya kuweza kuendesha shughuli zao kutokana na sheria ya muziki kufungwa saa sita.

Akizungumza na Wamiliki wa Bendi na Wanamuziki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watu hao kuunda kamati ya kuona jinsi watavyoweza kubadili sheria kutokana na mazingira ya sasa.Makonda amesema kuwa Watu wenye bendi wanamchango mkubwa katika pato la taifa kutokana na vinywaji kunywewa katika kumbi hizo wakati bendi hizo zikifanya kazi.

Aidha amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa watu wafuate sheria na amri zikitolewa watu wakubali na sio kila mtu kuamuka kufanya yake pamoja na kuangalia haki ya mtu mmoja inayoadhiri watu wengine

Amesema katika watu wanaofanya biashara hiyo wanatakiwa kuangalia katika vipengele moja ni ya muda gani wa kufanya biashara ,wamiliki wa baa ni muda gani wanaweza kuanza , wapi watu bendi wanaweza kufanya muziki.

Makonda amesema kuna vitu vya kuangalia katika kufanya biashara hiyo kuwa ni sehemu gani watapiga na mazingira je kuna hospitali,shule ,kanisa, msikiti.Amesema kamati lazima iwe na majibu ya vitu ambavyo ni vya msingi katika kuendesha shughuli zao bila kuathiri watu wengine.

No comments:

Post a Comment