Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa
mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Athuman Libanda baada
ya kuhitimu mafunzo ya siku 12 ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha vijana
wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa
JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi.
Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, .Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa
mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Bi. Joyce Shauza
baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali ya siku 12 yaliyoendeshwa na
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha
vijana wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa
NEEC, Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akiondoka katika ukumbi wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kufunga mafunzo ya siku 12 ya
wakufunzi wa somo la ujasiriamali mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali, Michael Isamuhayo. Mafunzo hayo
yaliendeshwa na NEEC.
Na Mwandishi wetu.
Jumla ya wakufunzi 53 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali na kutunukiwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa muda wa siku 12 na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Mafunzo hayo yalifanyika katika kambi ya Mgulani na kuhusisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Pwani.
Akikabidhi
vyeti hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi,
Ajira Vijana na Walemavu,Bi.Jenista Mhagama alisema wakufunzi hao wana
wajibu wa kuwafundisha somo la ujasirimali vijana wanaojiunga na jeshi
hilo ili kupambana na tatizo la ajira nchini.
“Mafunzo
mliyopata yalilenga kuwawezesha mkawafundishe vijana ili baada ya hapo
waweze kujiajiri au kuajiri wengine,” alisema,Bi. Mhagama mwishoni mwa
wiki.
Alifafanua
kwamba kuwafundisha somo la ujasiriamali itasaidia kwenda sambamba na
soko la ajira katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, utalii, hoteli na
kwamba nguvu kazi kubwa ya vijana itakuwa inafanya kazi badala ya kukaa
tu na kupenda starehe.
Alisema
serikali ya awamu ya tano imejielekeza katika kuwezesha wananchi na
jeshi hilo lina nafasi kubwa ya kutumia fursa iliyonayo kusaidia kukuza
vijana ili kwa pamoja kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.
Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Brigedia Jenerali, Michael Isamuhayo
alisema jeshi limejipanga kuwafundisha vijana wanaopitia mafunzo hayo
ipasavyo ili wawe chachu ya kukuza vipato vyao na uchumi wa nchi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi.
Beng’i Issa alisema utoaji wa mafunzo hayo kwa wakufunzi wa vijana kwa
jeshi hilo ni utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Kupitia
mafunzo haya wakufunzi watapata fursa ya kwenda kuwafundisha vijana
kupata stadi na kushiri katika uzalishaji mali na kuendesha maisha
yao,”alisema,Bi. Issa.
Aliwahimiza
vijana wanaohitimu masomo wajiunge na mafunzo ya JKT kwa wingi na huko
watakutana na mafunzo hayo yanayolenga kuwajenga kujitegemea.
Kwa
mujibu wa program hiyo, kanda itakayofuata itakuwa ya Kati na Magharibi
itakayojumuisha mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Mwanza,”alisema.
Mafunzo yatafanyika katika kambi ya Makutopora, Dodoma, Mafunzo
hayo katika kanda ya Kusni yatafanyika Mafinga ambapo mikoa
itakayohusika itakuwa Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe.
Mafunzo
katika kanda ya Kaskazini yatafanyika katika kambi ya Mgambo mkoani
Tanga na kuhusisha mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro.
Tangu
kurejeshwa kwa utaratibu wa mafunzo ya vijana wa kujitolea mwaka 2001
idadi ya vijana wanaojiunga na JKT imeendelea kuongezeka kila mwaka.
Vijana
waliopita JKT hadi mwaka 2014 ni 104,594. Kati ya idadi hii, vijana
34,291 waliingia kwa mpango wa kujitolea ambapo asilimia 70 waliajiriwa
na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama.
Asilimia 30 inayobaki, sawa na vijana 2,000 wanarudi nyumbani kila mwaka, Mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi wanaotambuliwa kimataifa.
No comments:
Post a Comment