Mkurugenzi
wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile ambaye pia ni
meneja wa bondia Francis Cheka akimwaga sera baada ya kupitishwa
kuwania nafasi ya Ukatibu Mkuu kwa Chama Cha Soka cha Manispaa ya
Kinondoni (KifA)
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile (wa kwanza
kushoto) akiwa na bondia wake Francis Cheka wakati wa kukabidhi mkanda
wa ubingwa Super Middle kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Nape Nnauye (wa kwanza kulia).
Meneja
wa bondia Francis Cheka, Juma “Chief” Ndambile amesema kuwa ameamua
kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Cha Kinondoni (KIFA)
kwa lengo la kuendeleza mchezo huu katika manispaa hiyo.Uchaguzi Mkuu wa
Kifa umepangwa kufanyika Mei Mosi na utawashirikisha jumla ya wagombea
33 waliopitishwa na kamati ya Uchaguzi ya chama hicho.
Ndambile
ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni maarufu ya ulinzi yaAdvanced Security
Co. Limited alisema kuwa kabla ya kuamua kuwania nafasi hiyo, alifanya
uchunguzi wa kina na kugundua kuwa pamoja na Kinondoni kuwa na wachezaji
wengi wenye vipaji, tatizo kubwa ni uongozi.
Ndambile alisema kuwa Kinondoni ina wadau wengi wa mpira wa miguu,
lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna timu inayoshiriki LigiKuu ya
Tanzania Bara na kubaki na timu za daraja la kwanza, pili na madaraja
mengine ya chini.
Alisema kuwa Kinondoni ina timu nyingi sana za mpira wa miguu
ambazo zinaibua vipaji kutoka chini na wengine kuwa wachezaji wa
kutegemewa wa timu za Ligi Kuu na timu ya Taifa, lakini kutokana na
mfumo wa uongozi kuwa si mzuri, wachezaji hawa wanahamia timu nyingine
na kuzipandisha daraja kucheza ligi kuu na Kinondoni kubakia nyuma.
“Kungekuwa na uongozi bora ambao ungekuwa unafuatilia kikamilifu
wachezaji na klabu, leo tusungekuwa na timu mbili tu daraja la kwanza,
Friends Rangers na KMC zingekuwa ligi kuu na nyingi zingekuwa daraja la
kwanza, sisi tumekuwa mishumaa wa kutoa mwanga huku tukiteketea,”
“Siri kubwa ya kuondokana na hili ni kutafuta wadhamini kwa timu
zetu na kuboresha hali ya wachezaji, Kinondoni ni Manispaa tajiri
Tanzania kwa kutumia wadhamini, waachezaji wangepata vipato vizuri na
kupunguza kazi kwa viongozi kuhangaika huku na kule kusaka fedha za
uendeshaji wa timu,” alisema Ndambile.
Alifafanua kuwa mbali ya maslahi ya waamuzi, pia atahakikisha
kunakuwa na uhusiano mzuri na vyama vishirikishi katika soka kama
madaktari wa michezo, makocha, soka la vijana, soka la wanawake,
Suptanza na wadau wengine ili kujenga umoja wenye nguvu. Alisema kuwa
yeye yupo tayari kufanya kazi wadau wote wa mpira wa miguu pamoja na
kuhimarisha zaidi uhusiano wa serikali ya Manispaa ya Kinondoni na chama
kwani ndiyo nyenzo pekee ya kufikia hatua kubwa kabisa ya maendeleo.
“Sitakuwa kiongozi wa kukaa ofisini, kama mtendaji nitakuwa
mfuatiliaji wa kila jambo kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali ya Awamu
ya Tano ya Rais John Magufuli, tunahitaji kufanya kazi na si kutafuta
sifa,” alisema.Mbali ya Ndambile, wagombea wengine katika nafasi hiyo ni
Hashim Abdallah, Selemani Sufiani, Ramadhani Kampira, Funua Ally, Isack
Mazwile na Raymond Solomon.
No comments:
Post a Comment