Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, April 11, 2016

KIJIJI CHA OLBILI CHAKABILIWA NA NJAA.

Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

Na Woinde Shizza,Simanjiro.
KIJIJI cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

Wananchi wa kijiji hicho Zuhura Salim na Anna Lazaro wamesema kuwa uhaba huo wa chakula unatokana na kunyang`anywa maeneo waliyokua wanatumia kwa kilimo na kutumika kama ardhi ya malisho.

Wananchi hao waliandamana na mabango yao kuzunguka eneo la shamba hilo 
wameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi na wizara ya kilimo kuingilia kati mgogoro huo baina yao na wafugaji wanaogombea eneo hilo ambalo kwa zaidi ya miaka 24 tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2013 ambapo walizuiwa kutumia maeneo hayo ambayo walikua wakiyatumia kwa shughuli za kilimo cha kujikimu.

Eliud Jackson ni Mwanakijiji wa Olbili amesema kuwa licha ya kunyimwa
maeneo ya kulima pia mwaka huu hawakupata chakula cha msaada kama kata 
nyingine zilizopata mgao huo hivyo kuteseka na njaa wao na watoto wao 
,wamemuomba Rais Magufuli kutazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tilili Kingi Lomayani Laizer amesema kuwa 
baada ya kuzuiliwa kulima na Mtendaji wa Kata na Diwani aliyekua 
madarakani walifika katika ngazi za wilaya bila mafanikio hivyo 
 wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Manyara afike kutatua mgogoro huo ili 
kuwanusuru na baa la njaa.

“Nimefuatilia suala hili kwa Mwenyekiti,Mtendaji wa kata na Diwani
aliyemaliza muda wake bila mafanikio kwani wao ndio walitoa zuio la
 kutuzuia kulima katika maeneo haya ,inaonekana jambo hili linashikiliwa na wafugaji wenye fedha wanatumia fedha zao kuwanyanyasa wakulima” Alisema Laizer

Aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo,ardhi kufika katika kijiji
hicho na kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwani wamekua wakishindwa 

kuendesha familia zao kutokana na kutegemea kilimo kama shughuli ya 
kuwapatia chakula na kipato.

No comments:

Post a Comment