Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, April 12, 2016

DIWANI KATA YA MAVANGA AISIMAMISHA KAMATI YA MRADI WA UMEME KUPISHA UCHUNGUZI

 WANANCHI WA KATA YA MAVANGA WILAYA YA LUDEWA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOJA KWENYE MKUTANO HUO


 DIWANI WA KATA YA MAVANGA WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE MWENYE SHATI NYEUPE Emmanuel  Mangalalikwa NA MWENYE KOFIA NI AFISA MTENDAJI WA KATA HIYO


 WANANCHI WA MAVANGA WILAYA YA LUDEWA WAKIWA KWENYE MKUTANO NA KUULIZA MASWALI
ALIYEKUWA KATIBU WA KAMATI YA NISHATI YA UMEME KATA YA MAVANGA GEOFREY FUTE AKITOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KABLA YA KUSIMAMISHWA KWA KAMATI YAKE  KUTOKANA NA MAPUNGUFU YALIOJITOKEZA


 MIONGONI MWA WALIOKUWEPO KWENYE KAMATI YA MRADI WA UMEME




Wananchi Wa  Kata Ya  Mavanga Wilayani Ludewa  Wamelazimika Kuisimamisha Kamati Ya  Mradi Wa Nishati Ya Umeme   Wa Maji  Unaohudumia  Wakazi Wa Kata Hiyo Tangu Mwaka 2002 Ulipotekelezwa Kwa Ushirikiano Na Wafadhili  Baada Ya Uongozi Wa Kamati Hiyo Kutuhumiwa  Kutumia  Fedha Za  Mradi  Huo  Kwa Maslahi Yao Binafsi.

Wakizungumza Kwenye Mkutano Wa Hadhara   Wananchi Wa Kata Mavanga Wamesema  Wamelazimika Kuusimamisha Uongozi Wa Kamati Hiyo   Ili Kupisha Uchunguzi Zaidi Kufanyika Dhidi Ya  Fedha Za Mradi Ambazo Zimedaiwa Kutowekwa Kwenye Akaunti Ya Mradi  Huo.

 Hatua  Ya Kuwasimamisha Viongozi Hao Imetokana Na  Tume Ya Uchunguzi Iliyoundwa Na Diwani Wa Kata Hiyo  Kutoa Taarifa Za Uwepo  Upotevu Wa Fedha  Za Mradi  Wa  Umeme  Wa Maji Zikiwemo  Za Bili,Ununuaji Nguzo Hewa   Pamoja Na Kuwepo Kwa Mfumo Mbovu Wa Kutoingiza Kwenye Kitabu Manunuzi  Na Fedha Zinazozarishwa.

Diwani Wa Kata Ya Mavanga Wilaya Ya Ludewa  Emmanuel  Mangalalikwa  Ameunga Mkono Kuwasimamisha Viongozi Wa Kamati Ya Mradi Wa Dishati Ya Umeme Kata Ya Mavanga  Kwaajili Ya Uchunguzi Zaidi Kutokana Na Malalamiko  Ya Wananchi  Huku Akisema Kamati Iliufanya Mradi Huo Kama Mali Ya Mtu Binafsi  Kinyume Na Sheria.

Akizungumza  Mara Baada Ya Kumalizika  Mkutano  Wa Hadhara Aliyekuwa Katibu Wa Mradi Wa Nishati Ya Umeme  Wa Maji Kata Mavanga Geofrey Fute  Amekili Kuwepo  Mapungufu Ya Uendeshaji  Mradi Huo  Kwamba Kamati Hiyo Haina Utaalamu Wa Kuendesha  Na Kukanusha Baadhi Ya Malalamiko Ya Wananchi Huku Yenye Ukweli Akisema Yanaendelea Kufanyiwa Ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment