mwenyekiti wa kikundi cha tumaini bwana stimer
Mwanafunzi huyo ambaye ni yatima akipokea msaada kutoka kwa kikundi hicho
kikundi cha tumaini baada ya kuwasili hapa kinajiandaa kukabidhi msaada kwa wanafunzi yatima na wenye wazazi wasiyojiweza
wanafunzi ambao wanategemea kupokea misaada Kutoka kwa wasamalia mbalimbali kama kikundi cha tumaini
mwenyekiti wa mtaa wa Nazareth John Mtitu akikabidhi mahitaji kwa watoto yatima Katika Mtaa wa nazareth
picha ya pamoja na wanafunzi waliopatiwa msaada huo na kikundi cha tumaini
Jumla Ya Wanafunzi Yatima Na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu 19 Wa Shule Ya Msingi Nazareth Kata Ya Mjimwema Mjini Njombe Leo Wamepatiwa Msaada Wa Mahitaji Mbalimbali Ya Shule Wenye Thamani Ya Shilingi Laki Saba Uliotolewa Na Kikundi Cha Tumaini Kilichopo Mtaa Wa Kambalage Eneo La Uyelevale.
Wakizungumza Mara Baada Ya Kukabidhiwa Msaada Huo Baadhi Ya Wanafunzi Wa Shule Hiyo Wameshukuru Kikundi Hicho Kwa Kuwasaidia Mahitaji Hayo Na Kuomba Wadau Wengine Kujitokeza Kusaidia Makundi Ya Watoto Ambao Wazazi Wao Hawana Uwezo Wa Kuwapatia Mahitaji Ya Msingi Ya Shuleni.
Aidha Wanafunzi Hao Wamesema Wengi Wao Hawana Wazazi Wote Yaani Baba Na Mama Ambapo Wanaishi Na Bibi Zao Ambao Baadhi Yao Uwezo Wa Kuwahudumia Mahitaji Yote Ya Shule Na Nyumbani Umekuwa Ni Mdogo Jambo Ambalo Linasababisha Baadhi Yao Kukosa Sare Za Shule .
Akizungumza Kwa Niaba Ya Wazazi Wakati Wa Kukabidhi Msaada Huo Uliotolewa Na Kikundi Cha Tumaini Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Nazareth John Mtitu Amepongeza Jitihada Za Kuwasaidia Watoto Hao Zilizofanywa Na Kikundi Hicho Na Kusema Kuwa Hata Siku Nyingine Wanakaribishwa Kutoa Misaada Mingine Kwa Watoto Hao.
Akizungumza Kwa Niaba Ya Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Mwalimu Wa Taaluma Bi. Flora Mligo Ameshukuru Kwa Msaada Uliotolewa Na Kuwataka Wanafunzi Kusoma Kwa Bidii Ili Kuwapatia Moyo Wadau Wa Elimu Wanaoendelea Kuwasaidia Mahitaji Kama Kilivyofanya Kikundi Cha Tumaini Na Kutaka Wadau Wengine Kuiga Mfano Huo.
Wakizungumza Mara Baada Ya Kukamilisha Zoezi La Kukabidhi Msaada Huo Baadhi Ya Wanakikundi Wakiongozwa Na Mwenyekiti Wao Daniel Stimer Wamesema Kikundi Hicho Kimwkuwa Kikichangishana Pesa Kila Mwaka Na Kutembelea Baadhi Ya Makundi Ya Watoto Yatima Kutoa Misaada Mbalimbali Nakwamba Wananchi Nao Watambuwe Umuhimu Wa Kusaidia Makundi Hayo.
No comments:
Post a Comment