NAIBU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wanataalum wa sekta ya afya kuacha
mara moja vitendo vya kupokea na kuomba rushwa kwani endapo watabainika
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Dk.
Kigwangalla emesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati
wa ufunguzi wa kuadhimisha siku ya kinywa na meno duniani yaliyofanyika
katika viwanja vya shule ya tiba ya kinywa na Meno, Muhimbili.
Ambapo amesema kuwa kwa utawala huu wa sasa Serikali ya awamu ya tano ni dhama nyingine na hawatamvumilia mtu.
“Ninaona
tu, bado kuna wachache wanaojihusisha na vitendo vya kuomba rushwa hapa
na pale. Kwa dhama hizi ukikutwa hatutakuurumia na hatutamuurumia mtu
kwa hili. Tunapaswa kuweka maslai mapana kwa wananchi tunaowahudumia
kwenye mioyo yetu” alieleza Dk. Kigwangalla.
Maadhimiho
hayo kwa mwaka huu yenye kauli mbiu “Afya njema ya kinywa ni afya ya
mwili mzima” kilele chake kinatarajiwa kufikia tamati Mkoani Morogoro
ambapo kwa siku zote hizi hadi kilele, Madaktari watatembelea shule
maalum kadhaa za ikiwemo ya Mtoni Maalum, Sinza Maalum, Buguruni Maalum
na zingine za Mkoa wa Shinyanga na Morogoro ambapo pia watafanya
uchunguzi na matibabu ya bure katika siku zote hizo.
Awali
katika ufunguzi huo, kulitanguliwa na matembezi maalum ya KM 10,
yaliyoongozwa na Naibu Waziri Dk. Kigwangalla ilikuhamasisha afya njema
ya kinywa na mwili katika mapambano hayo.
Matembezi
maalum ya ufunguzi wa siku ya maadhimisho ya kinywa na meno
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yakipita eneo la Maktaba Kuu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla (katikati) aliyeyaongoza matembezi hayo pamoja na
viongozi wengine waandamizi akiweo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Dk. Maseru (kushoto) na Rais wa Chama cha Madaktari wa
Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro wakiwasili
katika viunga vya Eneo la Chuo cha tiba ya meno Muhimbili baada ya
kutembea kwa umbali wa KM 10.
Baadhi
ya viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembea kwa
umbali mrefu wa KM 10 kama ishara ya kufungua maadhimisho ya siku ya
tiba ya meno duniani.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro akisoma hotuba maalum ya ufunguzi huo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba kwa wananchi na wageni waalikwa katika
tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba hiyo.
Mkuu wa Shule ya Kinywa na Meno, DK. Elison Simon akitoa hutuba yake katika tukio hilo.
Baadhi
ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania
(TDA) wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi, Dk. Hamisi Kingwangalla
wakati wa tukio hilo.
Baadhi
ya viongozi waandamizi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajia kufanyika Mkoani Morogoro Machi
20.2016, ambapo watatoa huduma bure ya tiba ya kinywa na meno. (Picha
zote na Andrew Chale).
No comments:
Post a Comment