KATIBU CCM MKOA WA NJOMBE HOSEA MPAGIKE AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
Halmashauri Kuu Ya CCM Mkoa Wa Njombe Imewataka Watumishi Wa Umma Kuyapokea Mabadiliko Ya Utendaji Kazi Na Kuacha Kufanya Kazi Kwa Mazoea Badala Yake Wafanye Kazi Kwa Uadilifu,Uwajibikaji ,Uhodari Wa Kazi Na Bidii Na Ufaanisi Kwa Lengo La Kuharakisha Maendeleo Kwa Faida Ya Watanzania Wote.
Rai Hiyo Imetolewa Na Katibu Wa CCM Mkoa Wa Njombe Hosea Mpagike Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Kikao Cha Ndani Cha Halmashauri Kuu Kilichodhamilia Kujadili Mambo Mbalimbali Ya Maendeleo Ya Chama Ikiwemo Kutoa Tathmini Ya Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Mwaka Jana.
Aidha Mpagike Amesema Miongoni Mwa Mambo Yaliopewa Kipaumbele Kwenye Kikao Hicho Ni Pamoja Na Watumishi Kufanya Kazi Kwa Uadilifu,Kujituma Na Uwajibikaji Kwa Manufaa Ya Watanzania Wote Ili Kuendana Na Kasi Ya Uongozi Wa Awamu Ya Tano Huku Katika Uchaguzi Huo Akisema Chama Cha Mapinduzi Kilishinda Kata 90 Dhidi Ya Wapinzani Wake Ambao Wameshinda Kata 17.
Mpagike Amesema Halmashauri Hiyo Pia Imepongeza Utendaji Kazi Na Utekelezaji Wa Ilani Wa Chama Hicho Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri Kwa Siku 100 Tangu Kuchaguliwa Ambapo Amefanikiwa Kupambana Na Maovu Nchini Ikiwemo Kukemea Vitendo Vya Rushwa,Ujangile,Madawa Ya Kulevya ,Uzemba Na Wizi Wa Mali Za Umma.
Amesema Swala Lingine Lililotajwa Na Halmashauri Hiyo Ni Pamoja Na Dr Magufuli Kuanza Kutekeleza Uboreshaji Elimu Kwa Kuondoa Ada Kwa Shule Za Msingi Na Sekondari Kuanzia Kidato Cha Kwanza Hadi Cha Nne Jambo Ambalo Limetajwa Kuwanufaisha Wazazi Waliokuwa Hawana Uwezo Wa Kupeleka Watoto Shule.
Kuhusu Miradi Ya Serikali Iliyoshindwa Kukamilika Kwa Kipindi Kilichopita Halmashauri Hiyo Imeagiza Kupewa Kipaumbele Cha Kukamilisha Kabla Ya Kuanza Miradi Mipya Kupitia Bajeti Za Serikali Zinazotengwa Ambapo Amesema Kuna Majengo Ya Shule,Zahanati Ambayo Nguvu Ya Wananchi Ilitumika Lakini Haikukamilika Ili Ku0koa Majengo Hayo Yasiharibike.
Kikao Hicho Cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa Njombe Kimefanyika Februari 13 Katika Ofisi Ya Chama Cha Mapinduzi Kikiwa Na Agenda Kuu Mbili Ikiwemo Kufanya Tathmini Ya Uchaguzi Mkuu Wa Rais ,Wabunge Na Madiwani Wa Mwaka 2015 Na Taarifa Ya Kazi Za Chama .
No comments:
Post a Comment