Monday, March 7, 2016
KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA NJOMBE MJINI LEO INAKWENDA KWA MARA NYINGINE KATIKA MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA-NJOMBE
SIKU CHACHE ZILIZOPITA KESI ILIPOKWENDA MAHAKAMANI HALI ILIKUWA HIVI
HAPA BAADA YA KUTOKA KAHAKAMANI MASHABIKI WA MLALAMIKAJI EMMANUEL MASONGA WANAKUTANA KUTETA KIDOGO NA WAKILI WAO
MASHABIKI WA MLALAMIKIWA NAO WALIKUWEPO NA HAPA NI KABLA YA KUINGIA MAHAKAMANI WANATETA KIDOGO
WAKILI WA MLALAMIKAJI ENOS EDWIN SWALE AKIWAELEZA KILICHOZUNGUMZWA MAHAKAMANI NA NINI CHA KUFANYIKA.
HII NI TAARIFA YA KIPINDI KILICHOPITA KESI ILIPOKUWA IMEKWENDA MAHAKAMINI NA KUAHIRISHWA HADI LEO TAREHE 8 MACH ,2016 INAKWENDA KUTOLEWA MAAMUZI.
Mahakama Kuu Kanda Ya Iringa Imeahirisha Kesi Ya Kupinga Matokeo Ya Ubunge Jimbo La Njombe Kusini Ya Mwaka 2015 Inayowakabili Watuhumiwa Watatu Mbunge Wa Jimbo Hilo Edward Franz Mwalongo,Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Iluminata Mwenda Na Mwanasheria Wa Mkoa Hilmar Danda Ambaye Alikuwa Msimamizi Wa Uchaguzi.
Kesi Hiyo Imeahirishwa Leo Kwa Mara Ya Tatu Baada Ya Mawakili Kushindwa Kufikia Mwafaka Juu Ya Hati Iliyowasilishwa Mahakamani Hapo Na Wakili Wa Mlalamikaji Enos Swale Ambayo Imepingwa Na Wakili Wa Serikali Apimack Mabrouk Aliyeiomba Mahakama Itupiliye Mbali Paragraph Nne Kwamba Hazina Hoja Za Msingi.
Akizungumza Mbele Ya Jaji Wa Mahakama Kuu Kanda Ya Iringa Jacob Mwambegele Wakili Wa Serikali Apimack Mabrouk Ambaye Anawatetea Watuhumiwa Wawili Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Njombe Na Mwanasheria Wa Mkoa Aliyekuwa Msimamizi Wa Uchaguzi Hilmar Danda Amesema Hati Hiyo Iliyowasilishwa Imekosa Sifa Kwa Kuwa Haina Tarehe,Muda Na Maneno Yaliyotumika Yanadhana Pana Zaidi.
Aidha Wakili Huyo Mabrouk Amesema Maneno Kama Leadership,Campen Team Wa CCM Walitembea Kata Kwa Kata Ama Nyumba Kwa Nyumba Nakwamba Hati Hiyo Imekosa Sifa Kwa Madai Haiweki Wazi Mahala Na Tarehe Ya Tukio Lilipokuwa Likitendeka.
Wakili Wa Kujitegemea Ambaye Anatetea Kesi Ya Mlalamikaji Enos Swale Amesema Hoja Za Wakili Mwandamizi Wa Serikali Hazina Msingi Na Haziwezi Kuondoa Baadhi Ya Paragraph Ambazo Zimeainishwa Kwenye Hati Hiyo Ya Mlalamikaji Nakwamba Wametaja Magari Na Namba Zake Hivyo Mahakama Haiwezi Kuondoa Baadhi Ya Paragraph Hizo Kwa Kuwa Hoja Za Wakili Wa Serikali Hazina Msingi.
Jaji Wa Mahakama Kuu Kanda Ya Iringa Jacob Mwambegele Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Tarehe 8 Mwezi Wa Tatu Saa Nne Asubuhi Jaji Wa Mahakama Hiyo Atakwenda Kutoa Maamuzi Ya Kesi Hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment