Na Mwandishi Maalum, New York
Jumuiya ya Kimataifa imezitaka pande zinazopinga Nchi Burundi, kumpatia ushirikiano wa kutosha ,Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuratibu majadiliano ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchi humo.
Pamoja na pande zinazopingana kutakiwa kufanya hivyo kwa moyo mmoja, pia Taasisi za Kimataifa na Kikanda ukiwamo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, pamoja na wadau wengine wametakiwa pia kumuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Wito huo umetolewa siku ya Jumatano, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakati Wajumbe wa Burundi Configuration walipokutana katika kikao chao na kujadili hali ya kisiasa na kiusalama inavyoendelea nchi Burundi kufuatia ziara iliyofanywa na Mwakilisji wa Kidumu wa…… Balozi Jurg Lauber ambaye ni Mwenyekiti wa Burundi Configuration.
“Tunakaribia uteuzi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa mratibu wa mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. Tunatoa wito kwa pande zinazopingana nchi humo, serikali na vyama vya kiasa kumpatia ushirikiano bila ya mashari yoyote” akasema Mwakilishi wa Marekani.
Naye Mwakilishi wa Kudumu wa Ubeligiji, Balozi Benedicte Frankinet. Pamoja na kueleza kwamba ujumbe wake unawasiwasi kuhusu taarifa za kuendelea kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mbinyo kwa vyombo vya habari na uhuru wa watu kutembea.
Amesema .“ Rais Mstaafu wa Tanzania , Benjamin Mkapa, anauzoefu mkubwa na wa hali ya juu katika uratibu na utafutaji ufumbuzi wa migogoro ya kisiasa, ujumbe wangu unakaribisha uteuzi wake, hapana shaka ataratibu na kusimamia majadiliano jumuishi yatakayohusisha wadau wote wanaopingana nchini Burundi wakiwamo pia wajumbe wa asasi zisizo za kiserikali”.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa Netherland, Balozi Karel Van Oosterom, amesema ujumbe wake pia unakaribisha uteuzi wa Rais Mkapa, na kwamba pande zinazopinga nchini Burundi zinatakiwa kuitumia fursa ya uteuzi wa Mkapa kurejea katika meza ya majadiliano ambayo yatakuwa jumuishi na huku akizisihi pande hizo kutotoa masharti ya aina yoyote ile.
Naye Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda, pamoja na kukaribisha uteuzi wa Rais Mstaafu Mkapa ambaye amesema ana uzoefu mkubwa na wanaimani naye, alimshukuru pia, Rais John Pombe Magufuli kwa kumteua Mkapa.
Karibu wajumbe wote waliochangia majadiliano kuhusu hali ya Burundi walikaribisha na kupongeza uteuzi wa Mkapa huku, Mjumbe wa Nigeria pamoja naye kuunga mkono uteuzi wa Mkapa. Alisisitiza pia kwamba Majadiliano jumuishi ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu nchini Burundi yanapashwa kumilikiwa na Warundi wenyewe.
Akatahadharisha kwa kusema kwamba, mashinikizo kutoka nje ya Burundi hayana nafasi katika mchakato huo na kwamba hali hiyo ikiruhusiwa inaweza siyo tu kuathiri majadiliano hayo lakini pia itakuwa ni kuwaingilia wananchi wa Burundi.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi akichangia majadiliano hayo, yeye ametaka ushughulikiaji wa hali tete ya kisiasa na kiusalama uende sambamba na uondoajji wa vikwazo vya kiuchumi kwa Serikali ya Burundi.
“ Hakuna matinki ya kutia msisitizo wa kuitaka serikali ya Burundi kutekeleza mambo kadha wa kadhaa yakiwamo ya ukiukwaji wa haki za binadamu, pasi kuzungumzia hali mbaya ya uchumi na kijamii inayoikabili Burundi na watu wake. Akasema Balozi
Nakusisitiza . “Tunapojadili hali ya usalama tujadili basi na uondoaji wa vikwazo vya kiuchumi kwa sababu mambo haya yanakwenda kwa pamoja. Njia sahihi ya kusaidia mchakato wa kutafuta amani ya kudumu nchini Burundi ni kwa sisi sote tulio katika meza hii kufanya kazi kwa pamoja na katika namna inayoeleweka”.
Vile vile Balozi Manongi ambaye Tanzania ni mjumbe wa Burundi Configuration ambayo ni sehemu ya Kamisheni ya Ujenzi wa Amani ( Peace Building Commission) amesisisiza wananchi wa Burundi kumiliki mchakato wa majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi yao.
Hoja ya kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi, Warundi kumiliki majadiliano yao, pia imeungwa mkono na mjumbe wa China ambaye amesema Haki za binadamu zinahusu pia haki ya kupata maendeleo na kwamba Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuisadia Burundi kiuchumi ili wananchi wapate maendeleo ambayo ni haki yao.
No comments:
Post a Comment