Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Assumpter Mshama akizungumza mbele ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wanging’ombe (WINGISA), Philemon Luhanjo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Mwenyekiti wa Bodi ya
WINGISA, Philemon Luhanjo, Meneja WINGISA, Inj. Najib Asumbwile (mwisho
kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Maji Vijijini, Inj. Jackson Mutazamba
(mwisho kushoto) pamoja na wafanyakazi wa WINGISA.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akitembelea chanzo cha maji cha Fukulwa, Wilaya ya Makambako.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga na
Mkuu wa Wilaya ya Makambako, Sarah Dumba wakiwa kwenye eneo la ujenzi la
Bwawa la Tagamenda, Wilaya ya Makambako.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akizungumza na wananchi wa Manga, Wilaya ya Makambako.
………………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Inj. Gerson Lwenge leo ametembelea Wilaya za Wanging’ombe na Makambako
mkoani Njombe na kujionea hali ya utekelezaji wa miradi ya maji
kulingana na ahadi ya Mhe. Rais, John Magufuli katika kampeni zake za
urais.
Aidha, ziara yake hiyo imelenga kuhakikisha kuwa miradi inayosuasua inatekelezwa na kuisha kwa wakati ili kutatua kero ya maji kwa wananchi kulingana na Sera ya Maji ya Mwaka 2002, kutimiza lengo la ifikapo mwaka 2025 wananchi wote mijini na vijijini wawe wanapata maji kwa asilimia mia.
Aidha, ziara yake hiyo imelenga kuhakikisha kuwa miradi inayosuasua inatekelezwa na kuisha kwa wakati ili kutatua kero ya maji kwa wananchi kulingana na Sera ya Maji ya Mwaka 2002, kutimiza lengo la ifikapo mwaka 2025 wananchi wote mijini na vijijini wawe wanapata maji kwa asilimia mia.
Vilevile, Inj. Lwenge alifika
kwenye Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Wanging’ombe (WINGISA)
kujionea utendaji wa mamlaka hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wake kwa
nia ya kuboresha utendaji wake.
No comments:
Post a Comment