Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, February 25, 2016

Waziri Mkuu awataka Mawaziri kuzingatia Maadili

1
Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa,Majaliwa akizungumza na mawaziri na manaibu waziri wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
2
Waziri ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
4
Kamishna Tume ya Maadili kwa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu salome Kaganda akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
5
Baadhi ya Mawaziri na manaibu Waziri wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda ikiwa ni ishara ya kuonesha uzalendo kwa nchi kabla ya kuanza semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
7
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi Virginia Blaser akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe huku mawazili wengine wakisililiza mazungumzo hayo.
8
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimsikiliza  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. JumanneMaghembe kabla ya kuanza kwa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam katikati ni Waziri ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
9
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza jambo pamoja na mawaziri wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam ,kulia ni  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Uratibu, Bunge,Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama(Kulia na katikati ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi.
10
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Hamad Masauni  kushoto  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina huku mawazili wengine wakupitia makabrasha yao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
11
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo kwa mawaziri na manaibu iliyotolewa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewaasa Mawaziri na Manaibu Waziri kuzingatia sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma kwani maadili ni nyenzo  kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
Mheshimi wa Majaliwa ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya Maadili kwa Mawaziri na Manaibu Waziri inayolenga kuwajengea uwezo mkubwa yanamna kiongozi wa utumishi wa umma anavyotakiwa kutekeleza majukumu yake bila kukiuka maadili.
“Chimbuko la Maadili ya Utumishi wa Umma ulianza tangu siku nyingi na umekuwa ukitajwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo katika Katiba ya nchi ya mwaka 1977, Sheria za Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishiwa Umma,”alisemaMajaliwa.
Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo WaziriMkuu alisisitiza kuwa Semina hiyo siyo semina elekezi kwa viongozi hao kama jinsi imekuwa ikijadiliwa katika mitandao ya kijamii, bali ni semina inayolenga kutoa mwongozo wa maadili ya viongozi wa umma na utekelezaji wa Hati ya Ahadi ya Uadilifu na mada katika semina hiyo zitahusu masuala ya maadili tuu.
Kwa upande wa Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma amesema semina ya maaadili kwa viongozi ni jukumu la Sekretariati ya maadili kuandaa kwani hiyo ni sehemu ya majukumu ya Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma na wao ndiyo wenye wajibu wakuhakikisha viongozi wa utumishi wa umma wanazingatia maadili.
“Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma inamamlaka ya kufanya uchunguzi kwa kiongozi yoyote wa umma atakayesikika kukiuka maadili kama kiapo cha ahadi za uadilifu kinavyosema,”alisema Jaji Mstaafu Salome.
Aidha Kamishna wa Maadili huyo aliendelea kusema Ofisi ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya rasimali fedha ambapo wanazaidi ya miaka mitatu wameshindwa kufanya uhakiki wa mali za viongozi pamoja na uchunguzi kutokana na changamoto hiyo.
Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na Shirika la USAID.

No comments:

Post a Comment