Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi
za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo
akifungua zoezi la utoaji damu linaloendelea leo katika viwanja vya
Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Zoezi hilo
linaendea hadi kesho.
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi
za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo
akiongoza zoezi la utoaji damu leo katika viwanja vya Karume mkabala na
Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Nemganga Kizega akipima afya ya Mkazi wa Vingunguti
jijini Dar es Salaam, Merry Kapande aliyefika leo kuchangia damu katika
viwanja vya karume mkabala na ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Wanafunzi wa Tambaza wakichangia damu leo katika zoezi linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.
Dk Patrick Shao ni mmoja wa
wafanyakazi wa Muhimbili ambaye alifika katika viwanja hivyo kwa ajili
ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari
ya Tambaza na Jangwani wakisubiri kutoa damu leo katika viwanja wa
Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) leo emeendesha zoeti la kuchangia damu katika viwanja vya Karume
jijini Dar es Salaam ambako watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu ili
kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Zoezi hilo limeanza leo asubuhi
na litaendelea hadi kesho. Wanafunzi wa Jangwani Sekondari na Tambaza ni
kati ya makundi yaliojitokeza kutoa damu.
Pia watu mbalimbali wamejitokeza
kwa wingi kutoa damu akiwamu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Praxeda Ugweyo, madaktairi wa
muhimbili na kijana Joseph Starford Mgoha aliyetembea kwa mguu kutoka
Mwanza hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Pombe
Magufuli kutokana na utendaji wake uliotukuka.
Katika zoezi hilo Dk Ogweyo
amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchagia damu ili kuokoa
maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Pia, amesema zoezi hilo litakuwa
endelevu na amewaondoa shaka Watanzania kwamba utoaji wa damu hauna
madhara yoyote kwa kuwa kabla ya mtu kutoa damu anaandaliwa kitaalamu
ili kufanikisha kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment