Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati
kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja
na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya
millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za
Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka
serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana .
Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro
kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja
na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya
millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za
Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka
serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana .
Magodoro
waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa
vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia
zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani
Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .
Wafanyakazi
wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja
na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya
millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za
Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukabidhi misaada kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh
Amina Masenza (kushoto) , ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa
vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia
zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani
Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .
Iringa,
Februari 17, 2016: Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea
nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na
mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi
kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa.
Vifaa
hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo
kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama
kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo
hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole
walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi
katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema
Kiswaga.Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na
mashuka 35.
Mvua
zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba zilisababisha watu
1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu
yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu
wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.
Msaada
kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango wake wa uwajibikaji
kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali
za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii
majanga yanapo ibuka.
No comments:
Post a Comment