Waziri
wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la
Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji
mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar
es Salaam kutokana utendaji usiolizisha.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Dionis Malinzi(kulia) akiongea jambo
na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye.Picha na
Daudi Manongi.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu
cha wageni wakati alipotembelea ofisi za Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) leo hii kuona utendaji wa Baraza hilo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua
uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya
baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.
Mhe.
Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema
katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua
changamoto walizonazo.“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo
vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema
Mhe. Nnauye.
Aliongeza
kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa
Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta
ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.Kutokana na utenguzi huo Mhe.
Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la
Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya
BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.
Vilevile,
Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa
ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta
chachu katika michezo nchini.Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu
wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi
nyingine wizarani.
No comments:
Post a Comment