Afisa
uhamiaji Mkoa wa Singida, Faith Ihano akitoa taarifa za kukamatwa kwa
wahamiaji haraamu kutoka nchini Ethiopia waliokuwa wakisafirishwa kwenda
Afrika ya kusini.
Watumishi wa idara ya uhamiaji Mkoa wa Singida waliofanikisha upatikanaji wa watu 15 ambao ni raia wa Ehiopia.
Wahamiaji haramu 15 waliokuwa wametoka Ethiopia wakisubiri katika
nyumba moja ya mtaa wa mitunduruni kusafirishwa kwenda Afrika ya kusini.
Na Jumbe Ismailly,Singida.
IDARA ya
Uhamiaji Mkoa wa Singida imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 45 raia
wa kutoka nchi za Ethiopia, Demokrasia ya Jamuhuri ya watu wa Congo
pamoja na Malawi kwa tuhuma za kuingia na kuishi nchini bila kuwa na
vibali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,
Ofisa Uhamiaji huyo wa Mkoa wa Singida, DSIS, Faith Ihano alisema
wahamiaji hao haramu raia wa nchini Ethiopia walikamatwa baada ya
kukutwa wakiwa wamefichwa kwenye nyumba ya mtu binafsi iliyopo kwenye
Mtaa wa Unyankindi, Manispaa ya Singida,mkabala na nyumba za Shirika la
Nyumba la Taifa(NHC).
Kwa mujibu wa Ihano wakati askari wa jeshi hilo wakiwa katika
doria kwa lengo la kukomesha wimbi la wahamiaji haramu hao linaloendelea
kujitokeza siku hadi siku,walikuwa wakisafirishwa kwenda nchini Afrika
ya kusini,wakitokea Jamuhuri ya Demokrasia ya watu wa Kongo, Malawi
pamoja na Ethiopia.
“Wahamiaji hawa haramu waliokamatwa idadi yao ni kumi na tano na
hao ni raia wa Ethiopia na kwamba wahamiaji hawa walikamatwa na askari
wa kikosi cha uhamiaji wakiwa katika doria na wahamiaji hawa walikuwa
wamehifadhiwa katika nyumba moja ya mtu binafsi”alifafanua Ihano.
Hata
hivyo kwa mujibu wa afisa uhamiaji huyo kwa sasa wanamshikilia mwenye
nyumba waliyokuwa wamehifadhiwa wahamiaji hao haramu kwa mahojiano zaidi
na pindi upelelezi wao utakapokamilika,hatua za kisheria zitaweza
kuchukuliwa dhidi yake.
Ofisa huyo wa uhamiaji hata hivyo alitumia fursa hiyo kutoa rai
kwa watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja
kwani idara ya uhamiaji inaendelea kufanya kila juhudi za kuwasaka wale
wote wanaowasaidia kuwaingiza nchini kinyume cha sheria na kuhakikisha
inawakamata na kuwachukulia hatua kali na za kisheria.
No comments:
Post a Comment