Baadhi
ya wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini wakiwa
katika mkutano wa kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya mwaka
2016/2017.
Baadhi
ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakiwa katika mkutano
wa kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya halmashauri hiyo ya
Singida vijijini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Bwana Simon Mumbee
akipitia taarifa zake anazotarajia kuwasilisha kwenye mkutano huo
maalumu kwa ajili ya kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya
2016/2017.
Diwani
Magreth Mangu (wa kwanza kutoka kulia) akibadilishana mawazo muda
mfuppi baada aya kumalizika mkutano maalumu wa baraza la madiwani
kupitissha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya Halmashauri hiyo ya
mwaka 2016/2017.
(Picha zote Na, Jumbe Ismailly)
BARAZA
la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Singida limepitisha mapendekezo
ya kufanyika kwa mabadiliko ya matumizi ya zaidi ya shilingi milioni 40
zilizotengwa kwa ajili ya kununua viburudisho na vitafuno wakati wa
vikao mbali mbali vya Halmashauri hiyo na badala yake fedha hizo
zielekezwe katika kutatua matatizo yaliyopo katika shule za sekondari za
bweni kwa wasichana.
Diwani
wa kata ya Ikhanoda,Hinga Mnyawi alitoa mapendekezo hayo kwenye mkutano
maalumu wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo uliokutana
kwa lengo la kupitisha mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa
2016/2017 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
“Jingine
mwenyekiti wakati afisa elimu sekondari akituaga amenikuna sana lakini
sisi naye tuliangalie sana hili,tunatenga fedha kwa ajili ya viburudisho
pamoja na vitafuno zaidi ya shilingi milioni arobaini nimesoma
hapa,zile hela kwa nini badala ya kula hapa tuzielekeze ziende
kuwasaidia watoto wa kike wanaosoma katika shule za bweni”alisisitiza
Mnyawi.
Aidha
diwani huyo alizitaja shule zitakazonufaika na kiasi hicho cha fedha
kilichotengwa kwa ajili ya viburudisho na vitafuno kuwa ni pamoja na
Kijota,Ughandi,Msange,Ikhanoda na Mwanamwema zilizopo katika Halmashauri
hiyo.
Hata
hivyo Mnyawi alibainisha kuwa umefika wakati kwa Halmashauri hiyo kulipa
deni la Kituo cha afya kilichojengwa katika Kijiji cha Ngimu kwa zaidi
ya miaka saba sasa lakini bado halijaezekwa.
Kwa
mujibu wa diwani huyo wakati wa kuanza ujenzi wa kituo hicho wananchi
walingia mkataba na mkandarasi kwa makubaliano ya kumlipa shilingi
milioni arobaini mara ujenzi huo utakapokamilika,jambo ambalo
wameshindwa kutekeleza.
“Kwenye
ukurasa wa kumi inasema uwepo wa madeni katika miradi viporo nakumbuka
kuna kituo cha afya kata ya Ngimu wananchi waliingia mkataba na
mkandarasi kwa makubaliano ya shilingi milioni arobaini kazi
itakapokamilika,lakini mpaka sasa bado hazijalipwa.”alibainisha Mnyawi.
Aidha
diwani Mnyawi hata hivyo aliweka bayana kwamba katika kudhihirisha
kwamba ujenzi wa zahanati hiyo umesahaulika aligundua kwamba hata kwenye
kabrasha walilokabidhiwa kujadili mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka
ujao wa fedha hakuna sehemu inayolitamka jengo hilo.
Wakichangia
hoja ya mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017
baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo walionyesha wasiwasi wao juu ya
fedha zilizotengwa kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya barabara.
Kwa
mujibu wa diwani wa kata ya Merya,Iddi Kijida kiasi cha shilingi milioni
39 zilizotengwa kwa ajili ya barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita
45 haziwezi kukamilisha matengenezo ya uhakika wa kuwawezesha wananchi
wanaolima na kusafirisha mazao ya biashara kama vitunguu kwenda kuuza
mazao yao kwenye soko la mjini Singida.
Naye
diwani wa kata ya Itaja,Paul Himida aliweka bayana kwamba kutokana na
Halmashauri hiyo kuwa na mahitaji makubwa ya fedha hivyo hawana budi
kwenda kusimamia kwa karibu makusanyo ya ndani ili waweze kufanikisha
kusaidia kwenye miradi viporo vilivyobakia katika mwaka wa fedha wa
2015/2016.
Akifungua
mkutano huo maalumu wa Baraza la madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Singida,Elia Dgha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi
juu ya umuhimu wa kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha wakati huu kwa
kulima mazao ya mzizi ikiwemo viazi na mihogo,mtama na uwele kwa mazao
ya chakula na alzeti na vitunguu kwa biashara yatakayowasaidia endapo
baa la njaa litawakumba kama ambavyo lilivyowakumba kwa mwaka wa
2015/2016.
Hata
hivyo Digha ambaye pia ni diwani wa kata ya Msange aliishukuru serikali
kwa kuipatia Halmashauri hiyo zaidi ya tani mia nne za chakula ambazo
zimewasaidia wananchi wake kukabiliana na upungufu wa chakula uliokuwa
ukiwakabili.
No comments:
Post a Comment