Chama
cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) wameiomba Serikali kuwasaidia
kumtafuta Bw. Said Abdalah Ismail (47) mkazi wa Kijiji cha Mbezi
Mlungwana Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa (TAS)
Josephat Torner alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa
hii ya kupotelewa na mwenzao.
“TAS
kwa kushirikiana na Shirika la Under The Same Sun (UTSS) tunaendelea
kufanya juhudi ya kumtafuta na juhidi zetu tunaomba Serikali ituunge
mkono” alisema Torner
Torner
aliongeza kuwa, Said alionekana kwa mara ya mwisho Januari 31 mwaka
huu katika Kijiji cha Mtipule alikokwenda kuuza mboga za majani na
baadae alionekana katika kilabu cha pombe ya kienyeji ambapo inasemekana
aligombana na wenzie waliokua wakinywa pamoja kabla hajaondoka kilabuni
hapo.
“Tunalitaka
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lile la Afrika Mashariki
kujadili kwa kina tatizo hili na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu pia
vyombo vya dola kuhakikisha wakatili hao wanatafutwa, wanakamatwa na
kufikishwa mbele ya sheria ili sisi wenye ualbino tuweze kuishi kwa
amani.” Alisema Torner.
Amesema
kuwa pamoja na juhudi za kumtafuta Said kuendelea taarifa ya kupotea
kwake ilipelekwa kituo cha Polisi Wilaya ya Mkuranga na kupewa RB namba
MKU/PE/05/2016 pia kituo kidogo cha polisi Kimanzichana kwa RB namba
KIM/RB/50/2016.
Aidha,
Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo ambapo jina la muuza
pombe pamoja na majina ya wale aliogombana nao tayari yamewasilishwa
polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa chama cha Albino wilayani Mkuranga mkoani
Pwani Hassan Kambangwa akizungumzia tukio amesema amelipokea kwa
masikitiko makubwa na kuiomba Serikali kuwachukua hatua kali za kisheria
wote waliohusika katika tukio hilo.
Kambangwa ametoa wito kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji kutafuta mbinu za kuzuia ukatili huo.
Ikumbukwe
kuwa tukio hilo kwa Bw.Said Abdalah Ismail ni la pili kwa kuwa aliwahi
kupatwa na mkasa wa kukatwa kiganja cha mkono akiwa mkoani Morogoro
miaka michache iliyopita.
No comments:
Post a Comment