Baadhi
ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa vyao kwa masaada wa watu wa
zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara baada ya bweni lao
kuteketea kwa moto.
Baadhi
ya wanafunzi wakiwa nje kusbiri utaratibu mara baada waliofanikiwa
kuokoa baada ya bweni lao kutektea kwa moto.Picha na David Nyembe
Moto
ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya
sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni
hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi
february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha
Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya
sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29
mwaka huu ambapo hakuna
Muonekano
wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara
baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira
saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na
ajali hiyo ya moto. .
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na
wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya
mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa mabweni ya
wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu.
Kamati
ya ulinzi na Usalama wilaya ya Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama
athari zilizotokea mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya
sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto uliosababishwa na hitilafu ya
umeme February 29 mwaka huu .
Afisa
elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akizungumzia athari zilizojitokeza
mara baada ya mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga
jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na hitilafu ya umeme majira ya
saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
No comments:
Post a Comment