MBUNGE WA JIMBO LA MAKAMBAKO NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJOMBE DEO SANGA MAARUFU KAMA JA PEOMPLE.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI KATIKA KIKAO CHA ROAD BOARD CHA MKOA WA NJOMBE.
MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE {CHADEMA] LUCIA MLOWE AKISHAURI BARABARA ZA KUINGIA MKOANI ZA WILAYA YA MAKETE,WANGING'OMBE,LUDEWA NA LUPEMBE KUTENGENEZWA KWA KIWANGO CHA LAMI.
MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMBE JORAMU HONGORI AKIHOJI BARABARA YA LUPEMBE KWAMBA KWANINI ISITENGENEAZWE KWA KIWANGO CHA LAMI ILI WAKAZI WA LUPEMBE WASAFIRI KWA URAHISI KUFUATA HUDUMA ZA MATIBABU NA KUSAFIRISHA MIZIGO YAO.
MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE KUSINI EDWARD FRANZ MWALONGO ALIYEEGAMA MWENYE KOTI JEUSI UPANDE WA KULIA
HII NI SAFU YA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WAKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
KUSHOTO KATIBU WA CCM MKOA WA NJOMBE HOSEA MPAGIKE NA KULIA NI MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE {CHADEMA }LUCIA MLOWE WAKIWA KWENYE KIKAO HICHO.
MBUNGE WA LUPEMBE JORAMU HONGORI AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENTINO HONGORI
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewataka Wananchi Kuwa Wavumilivu Katika Changamoto Zinazowakabili Za Barabara Zinazoingia Makao Makuu Ya Mkoa Zikiwemo Za Makete,Ludewa,Wanging'ombe Na Lupembe Ambazo Zibiri Kutengenezwa Kwa Kiwango Cha Lami .
Rai Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Wakati Akifungua Kikao Cha Roadboard Mkoa Wa Njombe Na Kusema Kuwa Barabara Ya Njombe -Makete Yenye Urefu Wa Kilomita 109 Na Barabara Ya Makambako -Songea Yenye Urefu Wa Kilomita 295 Zimefanyiwa Upembuzi Nyakinifu Na Usanifu Kwaajili Ya Kujenga Kwa Kiwango Cha Lami.
Aidha Dkt Nchimbi Ametaja Barabara Nyingine Za Njombe -Lupembe,Madeke Hadi Mfuji Mkoani Morogoro Yenye Urefu Wa Kilomita 125, Njombe -Ndulamo, Makete-Kituro-Kisyonje Yenye Kilomita 205,Itone-Ludewa-Manda Kilomita 2011,Njombe -Ramadhani-Iyayi Yenye Kilomita 74 Zote Hizo Zinasimamiwa Na Mkoa Huku Barabara Ya Makambako Songea Ikiwa Ni Ya Kufanyiwa Ukarabati.
Dkt Nchimbi Amesema Kuna Barabara Za Kufanyiwa Upembuzi Na Usanifu Wa Kiina Kuwa Ni Pamoja Na Barabara Ya Njombe -Iyayi Yenye Kilomita 74,Kibena Njombe-Morogoro-Mfuji Kilomita 125,Chimala -Matamba-Kituro Kilomita 51,Madaba-Mundindi-Mkiu Kilomita 46 Na Barabara Ya Madaba -Mavanga Ludewa Kilomita 40.
Kwa Upande Wao Baadhi Ya Wajumbe Wa Bodi Ya Roadbord Mkoa Wa Njombe Wameshauri Mambo Mbalimbali Ikiwemo Barabara Zinazounganisha Makao Makuu Ya Mkoa Kutiliwa Mkazo Wa Kutengenezwa Kwa Kiwango Za Lami Ili Kutatua Changamoto Zinazowakabili Wananchi Wa Maeneo Hayo Ikiwemo Akina Mama Kujifungulia Njiani.
No comments:
Post a Comment