Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akiteta jambo na
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista
Muhagama katika ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili umefunguliwa
leo na unafanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Vyombo
mbalimbali vya Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wa
Mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili
unafanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti,
Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Rehani Athumani akifuatilia mkutano
wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki uliofanyika
leo Jijini Dare s salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria
mkutano wa vyama vya mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na kati wakiwa
wamesimama kumuaga mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan
alipokuwa akifungua mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu
Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mawaziri na manaibu
waziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa
mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na kati
leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti katika
Mkutano wa Nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais amefungua rasmi mkutano huo leo katika Ukumbi wa Benki
Kuu.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu
Hassan ameshauri kurasimishwa kwa ajira zisizo rasmi ili ziweze
kuchangia katika pato na maendeleo ya Taifa kwa kukuza uchumi wa mtu
mmoja na wa Taifa kiujumla.
Ametoa ushauri huo Leo Jijini Dar
es salaam wakati akifungua mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii Afrika Mashariki na Kati amesema ili kuwezesha kuzalisha ajira
nyingi ni vyema kurasimisha ajira zisizo rasmi ili kutoa nafasi nyingi
kwa vijana kujiajiri na kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira barani
Afrika.
“Ili wananchi waweze kujiamini na
maisha yao ya baadae ni lazima wawe na imani na ajira zao pamoja na
hali nzuri ya kiuchumi,kukua kwa uchumi ndio njia rahisi inayowezesha
upatikanaji wa ajira.”
“Kuanzishwa kwa Mifuko ya Jamii
kumesaidia kuwainua wananchi kiuchumi,kijamii na inawalinda watu
wasipoteze ajira zao, na ndio sababu Mifuko hii inajulikana kama “haki
kwa watu wote” (Universal Right)” Alisema Mhe. Samia.
Ameongeza kuwa, ni lazima iundwe
mikakati mizuri ya kukuza uchumi ambayo itasaidia katika ukuzaji wa
biashara,uwepo wa bajeti yenye nguvu,kuwekeza katika miundo mbinu pamoja
na kuwa na mifumo mizuri ya kodi.
Aidha,amewaomba wanaohusika na utungaji wa sera za Mifuko ya Jamii kuzingatia sera zinazochochea ukuaji wa uchumi.
Mkutano huu ulihudhuriwa na
Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na
Kati ,Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Mkurugenzi wa Shirika la
Kazi Duniani (ILO) ,wakurugenzi wa mabenki na wawakilishi wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii.
No comments:
Post a Comment