KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE WILBROAD MUTAFUNGWA AKIZUNGUMZA NA MTANDAO HUU OFISINI KWAKE KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO LIKIWEMO LA USHIRIKINA LILOTOKEA KIJIJI CHA LUSISI KATA YA IGIMA WILAYA YA WANGING'OMBE.
HIKI NI KIJIJI CHA LUSISI
Akizungumza na Uplands Redio Kamanda wa Jeshi la P0lisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amekiri Kushikiliwa Kwa Wanandoa Hao na Kusema Kuwa Wanadaiwa Kuhifadhi Ndondocha (Misukule) Ambayo Ina Sadikiwa Kuwa ni Watoto Wao Waliofariki Mwaka Jana Kwa Kipindi Tofauti.
Kamanda Mutafungwa Amesema Kwa Mujibu wa Maelezo ya Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Lusisi Wamedai Kuwa Ndondocha Hao Wamekuwa Wakionekana Nyakati za Usiku Katika Mazingira ya Kutatanisha.
Katika Hatua Nyingine Jeshi Hilo Linaendelea Kufanya Uchunguzi Juu Ya Kifo Cha Mwananchi Mmoja Mkazi Wa Kijiji Cha Itebetale Makambako Elias Mwaise Mwenye Umri Wa Miaka 45 Ambaye Amekutwa Akiwa Amefariki Kwenye Mfereji Wa Maji Karibu Na Shamba Lake Ambapo Imedaiwa Kabla Ya Kifo Hicho Alikuwa Na Ugomvi Na Mke Wake.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amesema Tukio Hilo Limetokea Februari Tisa Mwaka Huu Baada Ya Ugomvi Na Mke Wake Ambao Ulitokana Na Mke Wake Kuzaa Mtoto Wa Nje Ya Ndoa Na Kusababisha Marehemu Kupatwa Na Jaziba Na Kuchoma Nguo Na Matandiko Wanayolalia.
Kamanda Mutafungwa Amesema Ugomvi Huo Ulianza Kutokea Tangu Tarehe 30 Ya Mwezi Januari Kutokana Na Kitendo Cha Mke Wake Kuzaa Mtoto Nje Ya Ndoa Na Kuamua Kuchoma Mashuka Na Magoro Ambapo Kifo Cha Marehemu Huyo Kinachunguzwa Ili Kujua Ukweli Wa Tukio Hilo Kama Ameuwawa Na Watu Ama Kajiuwa Mwenyewe.
Aidha Kamanda Huyo Amesema Wananchi Mkoani Njombe Wanatakiwa Kuonesha Ushirikiano Kwa Jeshi La Polisi Na Viongozi Wa Serikali Za Maeneo Wanapopatikana Kwa Kutoa Taarifa Zozote Za Uvunjifu Wa Amani Na Uharifu Ambao Utakuwa Unajitokeza Kwenye Maeneo Hayo.
Kwa Upande Wao Wajukuu wa Watuhumiwa Waliohojiwa na Uplands Redio Kuhusiana na Tukio Hilo Wamesema Kuwa Bibi Yao Anna Mgute Amekuwa Akiwaambia Kuwa Baba Zao Bado Wapo Hai ,Huku Baadhi ya Wananchi wa Lusisi Wakishauri Kutojihusisha naVitendo Vya Uvunjifu wa Amani Kuhusiana na Tukio Hilo .
Mtandao Huu Umemuhoji Mwenyekiti wa Kijiji cha Lusisi Leonad Ngibudzi Kuhusiana na Tukio Hilo Ambaye Hakuwa Tayari Kulizungumzia Suala Hilo Kwa Madai Kuwa Yeye Si Msemaji wa Kijiji Huku Katika Maelezo Yake Akikanusha Kuwepo Kwa Hali Hiyo.
No comments:
Post a Comment