Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, February 11, 2016

IDARA YA AFYA MKOA WA NJOMBE YAJIPANGA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KWA KUELIMISHA WANANCHI WASIKUTWE NA UGONJWA HUO.


 AFISA AFYA MKOA WA NJOMBE  MATHIAS GAMBISHI AKIZUNGUMZA NA MTANDAO HUU OFISINI KWAKWE  KUHUSIANA NA MIKAKATI YA KUUKABILI UGONJWA WA KIPINDUPINDU ENDAPO UTAINGIA MKOA WA NJOMBE

 KAIMU MGANGA MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT GABREIL NGOBEKO AKIZUNGUMZA JUU YA  KUWAPOKEA WAGONJWA  WATAKAOKUWA WAMEKUTWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU MKOA WA NJOMBE VIFAA TIBA,MAGARI YA WAGONJWA NA WATAALAMU WA HOSPITALI WALIVYOJIANDAA KUWAHUDUMIA WAGONJWA.



TAARIFA HII IMEANDALIWA NA Michael Ngilangwa Mmiliki Wa  Mtandao Huu Mawasiliano Ni, 0757092504/0678321772 Au michaelngilangwa@gmail.com

Badhi ya Wakazi Wa  Mkoa Wa Njombe Wameitaka Serikali Mkoani Njombe Kuweka Mpango Mkakati wa Kudhibiti Ugonjwa wa Kipindupindu Ambao Tayari Umeukumba Mkoa Jirani wa Iringa na Kusababisha Kifo cha Mtu Mmoja.

Wakiongea na Waandishi Kwa Nyakati Tofauti Wakazi Hao Wamesema Mkoa wa Njombe Huenda Ukakubwa na Ugonjwa Huo Kutokana na Baadhi ya Maeneo Yake Kuwa Machafu Huku Taka Zikiwa Zimezagaa Maeneo ya Ghuba za Kutupia Taka na Kuhatarisha Afya za Wananchi Ambao Nyumba Zao Zipo Karibu Ghuba Hizo.

Akizungumzia Mikakati ya Kukabiliana na Ugonjwa Huo Afisa Afya Mkoa wa Njombe Mathias Gambishi Amewataka Wananchi Kuzingatia Kanuni za Afya Ikiwemo Kunawa Mikono Kwa Sabauni Kabla ya Kula na Baada ya Kutoka Chooni, Kunywa Maji Safi Yaliyochemshwa na Kuhifadhiwa Sehemu Salama.

Aidha Gambishi Amesema Kuwa  Katika Kipindi Hiki Cha Mvua Kumekuwa Na  Magonjwa Mengi  Yakiwemo Ya  Magonjwa Ya Zika,Dengue,Malaria,Tafodi Na Ugonjwa Wa Kipindupindu  Ambapo Ugonjwa Wa Kipindupindu Unaambukizwa Kwa Kula Vyakula  Vichafu  Ambapo Wametoa Tahadhari  Maeneo Ya Barabara Kuu Za Iringa Mbeya,Kutuma Watalamu Kwaajili Ya Kutoa Elimu Juu Ya Ugonjwa Huo.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Gabriel Ngobeko Amesema Ili Kukabiliana na  Kipindupindu Amesema Tayari Wameandaa Dawa , Vifaatiba , Wataalam wa Afya wa Kutosha Kwa Ajili ya Kuwahudumia Wananchi Watakaougua Ugonjwa Huo, Huku Akielezea Namna Walivyojipanga Kutatua Changamoto ya Usafiri Na Kutaka Wahudumu Wa Vituo Ambavyo Havina Magari Kufanya Mawasiliano Mara Moja Kwa Wenye Magari.

Februari Sita Mwaka Huu Kumearifiwa Kulipuka Kwa Ugonjwa wa Kipindupindu katika Mkoa wa Iringa Ambapo Hadi Sasa Mtu Mmoja Amearifiwa Kufariki Huku Zaidi ya Wagonjwa 80 Wamelazwa Katika Kambi Maalum ya Kutibu Waathirika wa Ugonjwa Huo Iliyopo Katika Kijiji cha Mboliboli.;

No comments:

Post a Comment