Waziri
Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto), akizungumza na wanahabari
wakati akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), leo mchana.
Waziri
Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni
Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa.
Sumaye akisisitiza jambo
Sumaye (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wanaunda Umoja wa Katiba (UKAWA) baada ya kuondoka CCM na kujiunga na Chadema.
picha na fullshangwe blog DAR ES SALAAM
waziri mkuu wa awamu ya tatu fredrick sumaye ametangaza rasmi kukihama
chma cha mapinduzi CCMna kujiunga na chadema ni kupitia muungano wa
umoja wa katiba ya wananchi ukawa.
Akiongea na waandishi wa habari juu ya sababu zilizopelekea kuhama chama
cha mapinduzi waziri Fredrick Sumaye Amesema Inatokana na Yeye Kutokuwa
na Umuhimu Wowote Ndani ya CCM.
Akiongea mbele ya viongozi wakuu wa ukawa pamoja na mgomea urais kupitia
umoja huo edward lowasa sumaye amesema hafikirii kama kuondoka kwake
ndani ya ccm ni pengo kutokana na nafasi aliyokuwa nayo ndani ya chama.
Akizungumzia ujio wa waziri mkuu huyo wa awamu ya tatu ndani ya umoja wa
katiba ya wananchi ukawa mgombea uraisi wa chadema ambaye pia ni waziri mkuu mstafu wa awamu ya nne Edward Lowasa anasema kuwa watanzania wa leo wanataka mabadiliko.
Na mara baada ya kikao hicho kama kawaida yao viongozi hao wa ukawa
wakafunga kwa kuimba pamoja wimbo wa Taifa ili kuonyesha mshikamano.
No comments:
Post a Comment