Na Gabriel Kilamlya Njombe
Ikiwa Imebaki Siku Moja Tume Ya Taifa ya Uchaguzi NEC Kuzindua Rasmi Kampeni za Uchaguzi Mkuu Hapo Agosti 22 Mwaka Huu Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Kila Mmoja Anapaswa Kutambua Kuwa Zoezi la Uchaguzi ni La Mpito Lakini Amani Inatakiwa Kuendelea.
Kauli Hiyo Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Wakati Akizungumza na Vyombo Vya Habari Ofisini Kwake Juu ya Namna Jeshi Hilo Lilivyojipanga Kuelekea Katika Uchaguzi Mkuu.
Kamanda Mutafungwa Amesema Kwa Kuwa Suala la Kulinda Amani Ndani ya Nchi Halina Mjadala Basi Jeshi la Polisi Litahakikisha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu Unakwenda Bila Uvunjifu Wowote wa Amani.
Aidha Amesema Jeshi Hilo Limekuwa Likitoa Mafunzo ya Mara Kwa Mara Kwa Askari Wake Yatakayosaidia Kuhakikisha Amani Inakuwepo Muda Wote wa
Kipindi Cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu.
Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Ametoa Wito Kwa Jamii Kutambua Kuwa Kipindi Hiki Chote Kila Mmoja Anatakiwa Kuishi Kwa Kufuata Sheria ya Uchaguzi Huku Akivitaka Vyama Vyote Vya Siasa Vinavyohusika Katika Mchakato Huo Kuzingatia Muda wa Kufanya Kampeni Zake
Kumekuwepo na Tabia ya Kuibuka Kwa Vurugu Katika Kioindi Cha Kampeni za Chaguzi Mbalimbali Hapa Nchini Kwa Kile Ambacho Kimekuwa Kikielezwa ni Kushindwa Kupatikana Kwa Haki.
Suala Hilo Limekuwa Likielekezwa Kwa Jeshi la Polisi Kuwa Limekuwa Likishindwa Kutenda Haki na Badala Yake Kupendelea Baadhi ya Vyama Vya Siasa Kikiwemo Chama Cha Mapinduzi CCM Hususani Katika Kulinda Muda wa Kampeni Ambazo Kwa Mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Zinatakiwa Kuishia Majira ya Saa 12 Jioni.
Hata Hivyo Endapo Haki Itatendeka Kwa Vyama Vyote Vya Siasa Tunaamini Zoezi la Uchaguzi Mkuu Litakamilika Kwa Amani na Utulivu Mkubwa.
No comments:
Post a Comment