Friday, June 5, 2015
MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA YAFANYIKA LEO KWA WILAYA YA NJOMBE YAMEFANYIKIA MATIGANJORA
NGOMA YA ASILI IKIBURUDISHA KWA UZURI KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA SERIKALI YA KIJIJI HICHO MWENYE MZURA HUYO ANAITWA KASUTI
MTI UMEKWISHA KUPANDWA NA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA
NGOMA YA ASILI IKIBURUDISHA LEO
KAIM MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE BI.ELITA MLIGO AKISOMA RISALA FUPI KWA MGENI RASMI
MWENYE KOTI JEUPE NI MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Amekabidhi Zawadi na Vyeti Vya Utunzaji na Usafi wa Mazingira Kwa Kata za Ikuna na Kidegembye Kwa Kufanikiwa Katika Utunzaji na Usafi wa Mazingira.
Akizungumza Mara Baada ya Kukabidhi Vyeti na Zawadi Hizo Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Yaliyofanyika Kiwilaya Katika Kijiji cha Matiganjora, Bi. Dumba Amewataka Wananchi Kuendelea Kutunza Mazingira na Kuacha Tabia ya Kuchoma Moto Ovyo.
Nao Baadhi ya Wananchi Walioshiriki Maadhimnisho Hayo Wamesema Licha ya Kuaadhimisha Siku Hiyo Lakini Bado Wanakabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu wa Maji Safi na Salama Pamoja na Elimu ya Matumizi ya Vyoo Bora.
Awali Akisoma Risala Kwa Mgeni Rasmi Kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Bi. Elita Mligo Amesema Halmashauri Hiyo Inaendelea Kuwaelimisha Wananchi Katika Utunzaji na Usafi wa Mazingira.
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Huadhimishwa Mei 5 Kila Mwaka Ambapo Kwa Mwaka Huu Maadhimisho Hayo Kitaifa Yameadhishwa Mkoani Tanga Chini ya Kauli Mbiu Inasemayo ''NDOTO BILION SABA,DUNIA MOJA,TUTUMIE RASILIMALI KWA UANGALIFU''.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment