Friday, June 5, 2015
MWENYEKITI MTAA NJOMBE MJINI AKEMEA TABIA YA KUTUPA HOVYO CONDOM ZILIZOTUMIKA
Wananchi Na Wahudumu Wa Nyumba Za Kulala Wageni Mjini Njombe Wametakiwa Kuweka Mazingira Katika Hali Ya Usafi Kwa Kuhakikisa Wanatupa Taka Ngumu Kwenye Dampo La Taka Ikiwemo Kondomu Ili Kuepukana Na Milipuko Ya Magonjwa Ya Kuhara Yanayoweza Kujitokeza Kwa Watoto Na Baadhi Ya Wakazi Mjini Hapa.
Rai Hiyo Imetolewa Na Mwenyekiti Wa Mtaa Wa Gwivaha Bwana Denis Malekela Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Utupaji Hovyo Wa Kondomu Kwenye Mtaa Wake Na Kwamba Hali Hiyo Inatokana Na Uelewa Mdogo Uliopo Kwa Baadhi Ya Wahudumu Wa Nyumba Za Kulala Wageni Pamoja Na Baadhi Ya Wananchi Wasiyo Na Uelewa Wa Usafi Wa Mazingira.
Aidha Bwana Malekela Amesema Kuwa Kutokana Na Kuwepo Kwa Baadhi Ya Watu Wanaotupa Taka Ngumu Hovyo Serikali Ya Mtaa Huo Imelazimika Kuwaandikia Barua Baadhi Ya Wamiliki Wa Majengo Yaliyotelekezwa Bila Kukamilika Ujenzi Wake Na Pasipo Kufanyiwa Usafi Wa Kuondoa Nyasi Ili Kuondoa Maficho Ya Vibaka Ambao Wanaweza Kujificha Kwenye Maeneo Hayo Pamoja Na Kutupa Uchafu Wa Kila Aina.
Bwana Malekela Amepongeza Wananchi Wa Mtaa Huo Kwa Ushiriki M kubwa Wa Kuchangia Mchango Wa Taka Kiasi Cha Shilingi Laki Sita Za Mtaa Huo Ikiwa Laki Tatu Zimetakiwa Kuchangiwa Na Kila Mtaa Ambazo Zimekwisha Pelekwa Halmashauri Kwaajili Ya Kuzoa Taka Kwenye Vizimba
Kwa Upande Wake Baadhi Ya Wananchi Wa Mtaa Huo Waliozungumza Na Uplands Fm Mapema Leo Wamesema Kuwa Kitendo Cha Baadhi Ya Watu Kutupa Kondomu Hadharani Kinaweza Kusababisha Madhara Kwa Watoto Na Wakazi Wa Mtaa Huo Hususani Wanaotumia Maji Ya Bonde La Buguruni Huku Wakisema Huenda Taka Hizo Aina Ya Kondom Zikawa Zinatupwa Na Wahudumu Wa Nyumba Za Kulala Wageni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment