Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, May 24, 2015

WIKI YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUANZA RASMI KESHO MAKUMBUSHO YA TAIFA NA NYUMBA YA UTAMADUNI JIJINI DAR ES SALAAM



UNESCO inakusudia kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kusherehekea Wiki ya Ukombozi wa Bara la Afrika kuanzia tarehe 25 hadi
29 Mei 2015. Iwapo jambo hili litafana mwaka huu lirudiwe tena mwaka kesho na
hatimaye liwe ni la kila mwaka.


Wiki hii itaanza tarehe 25 Mei ya kila mwaka
husherehekewa kwa njia mbalimbali ndania na nje ya Bara la Afrika kukumbuka
siku ambayo viongozi wa nchi za kiafrika ambazo tayari zilikuwa huru walikutana
waka 1963 na kuanzisha Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika OAU). 


Shughuli
zilizopangwa kwa Wiki hii zinalenga kuongeza kiwango cha wananchi kutambua
umuhimu wa siku hiyo (MEI 25) ikiwa ni sehemu muhimu ya urithi wetu.


Mambo yanayokusudiwa ni kufanya maonesho, midahalo, matamasha na mashindano
ya kuandika insha kwa hapa Dar es Salaam na mikoani nje ya Dar es Salaam. 



Wiki
hii ni nyenzo muhimu ya utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara
la Afrika ambayo utekelezaji wake unasimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo.


No comments:

Post a Comment