Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, May 14, 2015

WANANCHI NJOMBE KUANZA KUCHANGIA TAKA KWA MIEZI MIWILI,BAJETI YA HALMASHAURI YA MJI MILIONI 80 ZIMEKWISHA

Halmashauri Ya Mji Wa  Njombe Ilitenga Kiasi Cha Shilingi Milioni 80  Kwaajili Ya Kuzolea Taka Kwenye Vizimba  Katika Kipindi Cha Mwaka 2014/2015   Ikiwa Ni Fedha Za Ndani Ya Halmashauri  Ambapo Fedha Hizo Zimetumika Kuanzia Mwezi July Mwaka Jana  Jambo Ambalo Limesaidia Wananchi Kupumzika Kuchangia Mchango Wa Taka  Kwa Kipindi Hicho.

Akizungumza Na Wananchi Wa Mtaa Wa Idundilanga  Mwishoni Mwa Wiki Iliyopita Diwani Wa Kata Ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Amesema Kuwa   Halmashauri  Ya Mji Wa Njombe  Kwa Kutambua Uwepo Wa Ongezeko La Uzarishaji Wa Taka   Imelazimika Kuongeza Kiwango Cha Fedha Kwenye Bajeti Ya Mwaka 2015/2016  Kutoka Milioni 80 Hadi Kufikia Milioni 108 Kwa Kipindi Cha Mwaka Wa Fedha  Wa 2015/2016.

Aidha Diwani Mtambo Amesema Kuwa  Katika Bajeti Ya Mwaka Wa Fedha Ya Mwaka 2014/2015  Fedha Iliyotengwa  Shilingi Milioni 80  Imekwisha Malizika Na Hivyo Halmashauri Inategemea Kutenga Fedha Kiasi Cha Fedha Hiyo Shilingi Milioni 108   Bajeti Itakayotengwa Kuanzia Mwezi June Na Hivyo Amewaomba Wananchi Kusaidia Kuchangia bFedha Ya Taka  Kwa Kipindi Cha Miezi Miwili Iliyobakia Wakati Wakisubiri  Halmashauri Itenge Fedha  Za Kuzolea Taka Hizo Kwenye Vizimba.

Bwana Mtambo Amekanusha Kauli Za Baadhi Ya  Watu Ambao Husema  Michango  Diwani Huyo Alizuia Wakati Akiingia Madarakani Na Kusema Kuwa  Yeye Alisema  Michango Isiyo Na Tija Itafutwa  Na Kiwango Cha Kuchangia Michango Ya Ujenzi Wa Miradi Mbalimbali Itashushwa  Ambapo Amesema  Ahadi Hiyo Imekwisha Kutekelezwa  Kwa Kushusha  Kiwango Cha Uchangiaji Kutoka Elfu 30 Hadi Kufikia elfu 6  Ya Ujenzi Wa   Shule  Na Majengo Mengine.

Kwa Upande Wao Wananchi Wamekubaliana Na Zoezi La Kuanza Kuchangia  Mchango Wa Taka Kwa Kipindi Hiki Kifupi Cha Muda Wa Miezi Miwili   Ili Kusaidia Halmashauri Uzoaji Wa Taka Hizo Wakati Ikiandaa Bajeti Ya Kuondoa Taka Kwenye Vizimba  Katika Bajeti Ya Mwaka 2015/2016.


No comments:

Post a Comment