Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kupitia Kitengo Cha Usalama Wa Barabarani Kwa Kushirikiana Na Wakufunzi Kutoka Chuo Cha VETA Songea Leo Limefanikiwa Kutoa Elimu Ya Usalama Barabarani Na Umuhimu Wa Kupatiwa Mafunzo Ya Udereva Kwa Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kwa Wananchi Wa Kijiji Cha Miva Kata Ya Luponde.
Wakizungumza Na Wananchi Wa Kijiji Cha Miva Kata Ya Luponde Wilayani Njombe Maafisa Usalama Wa Barabarani Sajent Braison Kambo Na Copro Hamad Hamiss Wamesema Kuwa Kufuatia Kuwepo Kwa Ongezeko La Vyombo Vya Moto Na Matukio Ya Ajali Jeshi Hilo Limelazimika Kuwatafuta Wakufunzi Kutoka Chuo Cha VETA Songea Ili Waende Kutoa Mafunzo Ya Udereva Kwa Wananchi Wote Huku Wamili Na Madereva Wakitakiwa Kujiandikisha Na Kupatiwa Mafunzo Hayo.
Maafisa Usalama Wa Barabarani Hao Sajent Kambo Na Hamiss Wamesema Kuwa Ili Wananchi Wa Kijiji Cha Miva Waweze Kuepukana Na Matukio Ya Ajali Ni Vema Kila Mwananchi Kuheshimu Matumizi Ya Watu Wengine Ya Barabara Ya Umma Na Kuwataka Wamiliki Na Madereva Wa Pikipiki Kuendesha Kwa Umakini Kwa Kuzingatia Watembea Kwa Miguu Nakwamba Sehemu Za Makazi Ya Watu Wanatakiwa Kutembea Siyo Zaidi Ya Mwendo Kasi Wa Km 50.
Akitoa Elimu Kwa Wananchi Wa Kijiji Hicho Mkufunzi Kutoka Chuo Cha Veta Songea Bwana Petter Mwipagi Amesema Kuwa Wananchi Wanatakiwa Kujikwamua Kiuchumi Kwa Kuunda Vikundi Vya Kiujasiliamali Ili VETA Songea Iwapelekee Walimu Wa Kutoa Mafunzo Ya Kutengeneza Nguo Za Batiki, Sabuni Na Mapambo Mbalimbali Huku Wamiliki Na Madereva Wakitakiwa Kujiandikisha Kwenye Ofisi Ya Kijiji Kwaajili Ya Kupatiwa Mafunzo Ya Udereva.
Kwa Upande Wao Wananchi Wa Kijiji Cha Miva Pamoja Na Kuhoji Maswali Mbalimbali Lakini Pia Wamepongeza Kwa Hatua Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Kwa Kushirikiana Na Chuo Cha Veta Songea Kwa Kuwapatia Elimu Ya Usalama Barabarani Na Kusema Kuwa Wako Tayari Kuanza Mafunzo Ya Udereva Ili Waweze Kuendsha Vyombo Vyao Vya Moto Pasipo Woga Wowote.
No comments:
Post a Comment