HUYU NI MKURUGENZI UTAFITI ,UTETEZI WA USHINDANI NA MIUNGANO YA KAMPUNI TUME YA USHINDANI {FCC} BWANA ALLAN MLULLA
AFISA MWANDAMIZI ,UTETEZI WA USHINDANI BWANA ALEX MMBAGA
SOMO LIMEWAKOLEA WAFAYANYABIASHARA NJOMBE
HAWA NI WASHIRIKI WA SEMINA HIYO AMBAYO INAENDELEA SASA HIVI KATIKA UKUMBI WA FM HOTEL -NJOMBE
MKURUGENZI UTAFITI ,UTETEZI WA USHINDANI NA MIUNGANO YA KAMPUNI TUME YA USHINDANI {FCC} BWANA ALLAN MLULLA AKISOMA RISALA FUPI KWA MGENI RASMI
MKUU WA MKOA WA NJOMBE BAADA YA KUWASILI KATIKA UKUMBI WA SEMINA LEO
MFANYABIASHARA PANGAMAWE AKIWA NA MFANYABIASHARA MWENZAKE BWANA CHAPWILA WAKIJIANDAA KUHOJI MASWALI KWENYE SEMINA HIYO BAADA YA HOTUBA YA MGENI RASMI
WASHIRIKI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI JUU YA USHINDANI WA KIBIASHARA
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKITOA HOTUBA YAKE LEO KATIKA UKUMBI WA FM -HOTEL BAADA YA KUPOKEA RISALA FUPI
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewataka Wafanyabiashara Mkoani Njombe Kuepukana Na Swala La Siasa Badala Yake Wafanye Biashara Kwa Umakini Na Kwa Mahesabu Makali Ili Kupata Faida Pamoja Na Kuondoa Chuki Za Kugombana Na Serikali.
Akizungumza Kwenye Semina Ya Siku Moja Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Nchimbi Amesema Kuwa Wafanyabiashara Hawataweza Kufanikiwa Endapo Hawataihusisha Serikali Kwa Kuwa Serikali Inatunga Na Kutafsili Sheria, Kutatua Baadhi Ya Changamoto Zinazowakabili Na Kutoa Vyombo Vya Kuwalinda Wafanyabiashara Hao.
Amesema Kuwa Wafanyabiashara Hao Watafute Njia Ya Kutatua Na Kujenga Mahusiano Mema Na Siyo Kugombana Na Serikali Na Kuweka Dhana Sahihi Ya Ushindani Wa Kibiashara Kwani Njombe Siku Chache Zijazo Itakuwa Ndiyo Lango Kuu La Maendeleo Kutokana Na Ongezeko La Wakazi Watakaokuwepo Kwenye Machimbo Ya Liganga Na Mchuchuma.
Awali Akisoma Risala Kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Utafiti Wa Ushindani,Utetezi Wa Ushindani Na Miungano Ya Kampuni Ya Ushindani FCC Bwana Allan Mlula Amesema Kuwa Tume ya Ushindani Ni Chombo Kinachosimamia Utendaji Wa Uchumi Wa Soko Kwa Nia Ya Kuhakikisha Misingi Ya Ushindani Nalindwa Na Kusimamiwa Ipasavyo Ili Kuwepo na fursa sawa Za Uchumi Miongoni Mwa Wazalishaji, Wasambazaji Na Walaji Ambao Ni watumiaji wa mwisho wa bidhaa na huduma mbalimbali.
Aidha Bwana Mlulla Amesema Kuwa Semina Hiyo Inalenga Kuwajenga Wote na kuongezea weledi wa namna ya kuboresha utendaji wa shughuli Zao kwa lengo la kuleta utendaji wa ufanisi na tija Katika uchumi wa Mkoa na Taifa Kwa Ujumla.
Kwa Upande Wake Washiriki Wa Semina Hiyo Wakiwemo Wafanyabiashara Na Wataalamu Wa Halmashauri Na Mkoa Wa Njombe Wamehoji Mambo Mbalimbali Ikiwemo Uhalali Wa Wafanyabiashara Za Usafirishaji Kuandika Kwenye Tiketi Kwamba Gari Likiharibika Kampuni Haita Husika Na Chochote Juu Ya Kuwasafirisha Ikiwa Wamelipa Nauli Na Kusema Kuwa Haki Inakuwa Wapi Majibu Ambayo Yamejibiwa Na Mtoa Mada.
No comments:
Post a Comment