Dk. Nchimbi alisema hayo jana wakati akizungumza na
waandishi wa nje ya ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe alipokuwa mgeni
rasmi katika kikao cha umoja wa wanawake wa CCM mkoani hapa kilichoenda
sambamba na semina ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).
Hatua inakuja baada ya waandishi wa habari kumtaka mkuu huyo
wa mkoa kulizungumzia tukio hilo, kufuatia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe,
Franco Kibona kwa muda wa wiki sasa
kupata kigugumizi cha kulizungumzia tukio licha ya kufuatwa mara kwa mara na
wahabari kutaka ufafanuzi.
Mkuu huyo wa mkoa, alisema ameunda tume hiyo ambayo itakuja
na kiini cha tukio la mauaji hayo yanayodaiwa kutekelezwa polisi, ambayo
yalisababisha wananchi wa Njombe kuandamana kupinga mauaji hayo na kusababisha
vurugu hali iliyowalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Pia Nchimbi alilaani mauaji hayo na kusema kuwa hayapaswi
kujitokeza tena kwa kuwa yanavuruga amani,
pamoja na kulaani waliochochea maandamano kwenda katika hospitali ya
kibena na hivyo kusababisha adha kwa wagonjwa.
“Tukio hili la mauji ninalilaani kwa kuwa limesababisha
kuvurugika kwa amani na kero kwa wagonjwa katika hospitali yetu ya kibena
lakini pia nalaani wanasiasa waliochochea wananchi kuandamana kwenda
hospitalini sehemu ambayo wagonjwa wanapatiwa matibabu na wanahitaji utulivu,”
alisema Dk. Nchimbi.
Alisema kamati aliyoiunda ina jumuisha viongozi wanne wa
madhehebu ya dini, na kwamba anatarajia kumpelekea majibu hivi karibuni mara
baada ya kumaliza uchunguzi wake ili kujua nini kiini cha tukio hilo la mauaji
na kuruhi, ambalo limeacha sintofahamu kwa wakazi wa Njombe hasa kutokana na
jeshi la polisi mkoani hapa kukaa kimya kwa kushindwa kulizingumzia hadi sasa.
No comments:
Post a Comment