Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Mabalozi wa Tanzania
unaofanyika katika hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
unajadili kwa kina namna ya kutekeleza dira mpya ya Sera ya Mambo ya Nje
ya Tanzania ili kuendana na mabadiliko ya Uchumi na Diplomasia Duniani
na kuleta tija nchini.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wakati wa
mkutano wa mabalozi wa Tanzania.Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Watatu Kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Nje Mh.Bernard Membe,Wanne kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Balozi Liberata Mulamula.(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment