RC NJOMBE AKITOA HOTUBA YAKE KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
MBUNGE VITI MAALUMU NA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE JINSIA NA WATOTO DKT PINDI HAZARA CHANA KUSHOTO KWAKE NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA KATIKATI NA RC NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI
PICHA YA PAMOJA NA RC NA VIONGOZI WENGINE WA CHAMA NA SERIKALI
PICHA YA PAMOJA YA RC NJOMBE NA WAWAKILISHI WA WANANCHI WILAYA YA NJOMBE
HAWA NI MADIWANI WA KATA ZA WILAYA YA WANGING'OMBE
Zaidi Ya Ajira Elfu 30 Zinatarajiwa Kutolewa Katika Miradi Ya Machimbo Ya Liganga Na Mchuchuma Mkoani Njombe Huku Wawekezaji Wa Kigeni Wakitarajiwa Kuwepo Wasiyo Pungua Elfu Sita Na Watu Wapatao Elfu 40 Wataingia Kwenye Machimbo Hayo Yanayopatikana Wilayani Ludewa.
Akizungumza Wakati Wa Ufunguzi Wa Semina Ya Siku Moja Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amesema Kuwa Tayari Wamekwisha Kuzindua Utaratibu Wa Kuhamasisha Watu Kutoa Elimu Ili Wananchi Wawe Tayari Kwaajili Ya Kufanya Uthamini Na Kulipa Fidia Kwa Wale Watakao Takiwa Kupisha Mradi Wa Liganga Na Mchuchuma.
Aidha Dkt Nchimbi Amesema Kuwa Akina Mama Wanapoandaliwa Katika Kufahamu Vipimo Mbalimbali Vya Bidhaa Pamoja Na Kujiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya Itawanufaisha Wazazi Na Watoto Wao Na Kuwa Na Afya Njema Na Kushiriki Kikamilifu Katika Kufanya Kazi Za Maendeleo Katika Miradi Ya Liganga Na Mchuchuma.
Amesema Kuwa Hatapenda Kuona Unga Wa Mahindi Unaingia Wilaya Ya Ludewa Kwa Maeneo Ya Liganga Na Mchuchuma Kutoka Nje Ya Mkoa Ikiwa Kuna Wananchi Wa Njombe Wanao Uwezo Wa Kufanya Kazi Hiyo Ya Kuanzisha Viwanda Na Kusindika Unga Kwaajili Ya Wafanyakazi Watakao Kuwa Wanafanya Kazi Kwenye Machimbo Hayo.
Dkt Nchimbi Amesema Kuwa Swala La Kujiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya CHF Ni La Lazima Kwa Kila Mwananchi Na Kwamba Asitokee Mtu Yeyote Atakaye Kwenda Kwa Wananchi Na Kuweza Kupotosha Wananchi Wasijiunge Na Mfuko Huo Na Kwamba Akina Mama Na Wananchi Wanatakiwa Kutokubali Badala Yake Wachangie Mfuko Wa Afya Wa CHF Kwa Shilingi Elfu 10.
Kwa Upande Wake Mbunge Was Viti Maalumu Na Naibu Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Wanawake Jinsia Na Watoto Dkt Pindi Hazara Chana Amesema Kuwa Lengo La Semina Hiyo Ya Siku Moja Kwa Wawakilishi Wa Wananchi Ni Kuwafanya Wananchi Waweze Kutambua Na Kujiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya Kwa Manufaa Yao.
No comments:
Post a Comment