Na Takdir Ali-Maelezo.
Wafanyakazi
38 waliodai kuachishwa kazi katika hoteli ya Rezidensi iliopo Kizimkazi
Wilaya ya kusini Unguja wameiomba Serikali ya Mapindyuzi Zanzibar
kuingilia kati mgogoro wa kuachishwa kazi na Mmiliki wa Hoteli hiyo.
Wamesema
wamesikitiswa na Uongozi wa Hoteli hiyo kuwaachisha kazi wafanyakazi
bila kuwepo kwa sababu yoyote ya msingi jambo ambalo ni kinyume na
Mikataba ya ajira waliokubaliana wakati wa uajiri.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Shirika la Utangazaji Zanzibar
(ZBC) kiongozi wa Wafanyakazi hao Mary Laurence Frank amesema wakati
wakiwa katika likizo walipata barua za kuachishwa kazi bila ya kujua
sababu za msingi.
Amefafanua
kuwa mara baada ya kupata barua za kuachishwa kazi tarehe 4/5/2015 na
kutakiwa kufanya makubaliano (cliarence)na Muajiri wao tarehe 8/5/2015
lakini cha kusikitisha wamekwenda Hotelini hapo kuanzia saa mbili hadi
saa kumi na mbili bila kuonana na kiongozi yoyote wa Hoteli hiyo.
“Tulikwenda
kufanya makubaliano (cliarence) ili watukabidhi mafao yetu ya kuvunja
mkataba na sisi tuwape vifaa vyao lakini wlifunga milango na
hawakuturuhusu kuingia ndani”Alisema Mary.
Amefafanua
kuwa madai ya kuachishwa kazi kutokana na msimu mdogo wa biashara (low
season) ni kinyume na makubaliano ya mikataba waliokubaliana na alisema
madai hayo hayana ukweli ndani yake.
Kwa
upande wake Mohd Ali Abdallah, ambae ni miongoni mwa waliochishwa kazi,
alisema wamiliki wa Hoteli hiyo wamekuwa wakiwadhalilisha kwa kiasi
kikubwa wafanyakazi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ikiwemo kuwatolea
maneno ya kashfa.
Amesema
wanachohitaji ni kukaa pamoja na Uongozi wa Hoteli na kuwapatia haki
zao za msingi kwa mujibu wa sheria na taratibu za Ajira ili haki iweze
kufanyika na kuiomba serikali kuwabana zaidi Wawekezaji wenye tabia ya
kuwadhalilisha wafanyakazi Wazalendo.
KWA HISAN YA JIACHIE BLOG
No comments:
Post a Comment