Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, May 23, 2015

KIONGOZI WA UPINZANI HUKO BURUNDI KAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOFAHAMIKA


Zedi Feruzi
Zedi Feruzi Kiongozi wa upinzani huko Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Bujumbura huku machafuko yakiendelea nchini humo. 
 
Zedi Feruzi, mkuu wa Chama cha Umoja wa Amani na Demokrasia UPD-Zigamibanga aliuawa Jumamosi usiku alipokuwa akiingia nyumbani kwake katika eneo la Ngagara. Mlinzi wake pia ameuawa katika tukio hilo.
Mwili wa Firuzi uliolowa damu ulipatikana nje ya nyumba yake huku walioshuhudia wakisema walisikia takribani milio 20 ya risasi na kwamba mlinzi wa pili wa Feruzi pia alijeruhiwa katika tukio hilo.

Kiongozi mwandamizi wa upinzani, Agathon Rwasa, amesema hakuna taarifa kuhusu ni nani aliyetekeleza mauaji hayo, lakini ameongeza kuwa Feruzi alikuwa anapinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Baada ya Feruzi kuuawa, vijana wa eneo hilo wameandamana na kufunga barabara za mtaa huo. Mauaji hayo yanakuja huku mgogoro nchini Burundi ukiendelea kutokota. Karibu watu 20 wamepoteza maisha tokea maandamano dhidi ya rais Nkurunziza yaannze katikati ya mwezi Aprili.



No comments:

Post a Comment