Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, May 23, 2015

KIKUNDI CHA MOVEMENT 4U CHA KABIDHI MSAADA WA MAHITAJI MBALIMBALI YA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA WALIOKO KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA COMPASSION FOUNDATION


WATOTO YATIMA WAKIWA KWENYE UKUMBI WAO WA CHAKULA  NA KUSIKILIZA VIONGOZI WA KUNDI HAO WALIOFIKA KUKABIDHI MSAADA HUO WA MAHITAJI MBALIMBALI BAADA YA KUGUSWA








 MJUMBE WA SEKRETARIETI MKOA MWALIMU JONEL NATHANIEL  KILEVA AKIZUNGUMZA NA WATOTO YATIMA WAKATI WA KUKABIDHI MSAADA HUO




PIA KWENYE KUNDI HILO KUNA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA AMAN TAWI LA TUMAIN IRINGA.


HUU NI MSAADA ULIOKABIDHIWA KWA WATOTO HAO YATIMA WA KITUO CHA COMPASSION FOUNDATION.



  HAPA WANAFURAHIA KUWAONA  WATOTO HAO YATIMA NA KUKABIDHI MISAADA NA KUZUNGUMZA NAO
WATOTO WAKIFURAHIYA  KUPATA MAZIWA  KWA RISHE BORA



WATOTO WANAOLELEWA KWENYE KITUO HICHO CHA COMPASSION FOUNDATION  WAKIWA NA KUNDI LA MOVEMENT 4U LILILOKWENDA KUKABIDHI MSAADA NA KUELEZA ATHMA YAO YA KWAMBA KIONGOZI BORA  AJAYE NI EDWARD NGOYAI LOWASSA




 STEWARD MKONGWA MJUMBE WA KUNDI HILO AKIWA AMEMUINUA MTOTO BAADA YA KUFIKA KATIKA  KITUO HICHO CHA KULELEA WATOTO YATIMA.

Kikundi Cha Movement 4U  Leo Limekabidhi Msaada  Wa Mahitaji Mbalimbali Ya

Nyumbani  Ikiwemo Sabuni,Mafuta Na Sukari Kwa Watoto Yatima Na Wanaoishi Kwenye

Mazingira  Magumu  Walioko Katika Kituo Cha Compassion Foundation   Wenye  Thamani

Ya Zaidi Ya Shilingi Lakini Moja Huku Wito Ukitolewa Kwa Wadau Wengine Wa Elimu

Kusaidia Makundi Ya Watoto Hao.

Wakizungumza Kabla Ya Kukabidhi Msaada Huo  Kwa Watoto Yatima Na Wanaoishi

Kwenye Mazingira Magumu  Katibu  Betha Mwalongo Na  Msaidizi Wake Wa Kundi La

Movement  4U  Ambaye Pia Ni Mwenyekiti Wa Muungano Wa Wasanii Wa Filamu Mkoa

Wa Njombe  Bwana  Adam Mbinda Amesema Kuwa  Lengo La Kwenada Katika Kituo

Hicho Ni Kutaka Kuunga Mkono Jitihada Za Baadhi Ya Wazazi Wanaokwenda Kusaidia

Watoto Hao Kwa Kukabidhi Msaada Huo.

Aidha Viongozi Hao Wa Kundi Hilo  Wamesema Kuwa Lengo Kubwa La Kuunda Kundi

Hilo Ni Kutaka Kutoa Elimu Kwa Wananchi Juu Ya Utawala Bora   Ili Ifikapo Mwezi

October Mwaka Huu Wananchi Wasikosee Kuchagua Kiongozi Bora  Kwani  Kundi Hilo

Limekuwa Likipita Kila Maeneo Kuhamasisha  Jamii  Na Kuona Umuhimu Wa Kuchagua

Kiongozi Bora Pasipo Kujali Itikadi Za Vyama.

Pamoja Na Kuhamasisha Wananchi Kutambua Kiongozi Bora Na Maana Ya Utawala Bora

Lakini Kundi Hilo Limesema Kuwa  Hamasa Kubwa Ambayo Kundi La Movement  4U 

Linaiifanya  Ni Kuhimiza Jamii Kuunga Mkono Makundi Ya Wananchi Wengine

Wanaounga Mkono  Kuchukua Fomu Ya Kugombea Urais  Edward Ngoyai Lowassa,

Mbunge Wa Jimbo La Monduri.

Kwa Upande Wao Wajumbe Wa Kikundi Cha Movement 4U Wamesema Kuwa Jitihada Za

Kutoa Elimu Kwa Viongozi Na Wananchi Juu Ya Utawala Bora Bado Zinaendelea Hata

Kwa Maeneo Mengine  Mijini Na Vijijini   Ili Kupata Mabadiliko Ya Viongozi Walio Bora

Ifikapo October  Mwaka Huu Huku Wakisisitiza  Edward Ngoyai Lowassa Kuchukua Fomu

Ya Kuwania Nafasi Ya Urais Ifikapo Mwezi October Mwaka Huu.

Awali Akizungumza  Kwa Upande Wake Mwalimu Wa Taaluma Katika Kituo  Cha Kulelea

Watoto Yatima Na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu Bwana  Oscar  Kihuru Amesema

Kuwa Shirika La Compassion Foundation Linahudumia Watoto Zaidi Ya Mia Nne  Yatima

Na Wanaoishi Kwenye Mazingira Magumu  Ambapo Waliopo Kwenye Kituo Hicho Wapo 

Zaidi Ya 30.

No comments:

Post a Comment