Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, April 18, 2015

WATU 18 WAFARIKI KWA AJALI YA GARI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

 

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHAMED Z. MSANGI AKIWA OFISINI KWAKE

Watu  18 Wamefariki katika ajali ya gari mkoani Mbeya baada ya basi dogo la abiria kuanguka na kutumbukia kwenye Mto Wilayani Rungwe.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahamed Msangi Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kwamba Kati ya Watu Hao 17 Wamefia Eneo la Tukio na Mmoja Amekufa Akiwa Hospitalini.

Kamanda Msangi Amesema Kuwa Tukio Hilo Limetokea Leo Majira ya Saa Tatu Asubuhi Ambapo basi hilo dogo limetumbukia bondeni katika eneo lenye mteremko mkali na kona.

Aidha Jeshi la Polisi Linaendelea Kufanya Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo na Kwamba Taarifa za Awali Kupitia Majeruhi wa Ajali Hiyo Zinaeleza Kuwa Dereva wa Gari Hilo Dogo Aina ya TOYOICE alikuwa na Mwendo Mkali 


Taarifa Zaidi Zinasema Polisi wanaendelea Kuchunguza chanzo cha ajali Hiyo na Kwamba Mashuhuda wa Ajali Hiyo wanadai dereva wa gari hilo alikuwa akiwakimbia madereva wengine waliotaka kumlazimisha aunge mkono mgomo wa utoaji huduma unaoendelea kwa safari za kati ya Mbeya na Kyela.

Imedaiwa Kuwa Hadi Sasa madereva wa mabasi ambayo kwa kawaida hutoa huduma kati ya eneo la Kyela na Mbeya mjini walikuwa katika mgomo na kwamba hawakufurahishwa na basi hilo dogo kuendelea kutoa huduma ndipo wakawa wanamfukuza hatimaye akashindwa kulidhibiti.

Ajali hiyo ni mwendelezo wa ajali mbaya za barabarani Zikihusisha magari ya abiria ambazo zimetokea Tanzania kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment