Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, April 26, 2015

JUST IN: gwiji la ukombozi wa afrika kusini brigedia jenerali hashim mbita afariki dunia leo dar es salam




Habari zilizotujia hivi punde zinasema Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam. 



Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku itayotajwa kesho na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.



Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.




Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.

No comments:

Post a Comment