Huyu ndiye Diwani wa kata ya Luilo pia mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa Mh.Mathei Kongo aliyenusurika kuchapwa bakora kutokana
na kupinga maendeleo
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya
Ludewa katika Mkoa wa Njombe Matei Kongo
ambaye ni diwani wa Kata ya Luilo jana
alinusurika kuchapwa viboko mkutanoni na Mbunge wa jimbo Ludewa Deo
Filikunjombe kutokana na Diwani huyo kutuhumiwa kuhamasisha wananchi kukataa
kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo kusafisha na kuchimba mashimo kwa ajili
ya umeme.
Filikunjombe alifikia hatua ya kumchapa
diwani huyo fimbo kama angekuwepo kwenye mkutano kutokana na wananchi wa kata
hiyo kumwambia kuwa diwani wao amekuwa akiwahamasisha kukataa kushiriki
nguvukazi ya kuchimba mashimo kwa madai kuwa serikali ndiyo yenye jukumu hilo
na kwamba kunafedha kwa ajili ya kazi hiyo siyo wananchi kuchimba.
‘’wananchi msinililie mimi jililieni
wenyewe na diwani wenu ambaye anazuia maendeleo yenu,fedha hizi siyo za
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa nimezitafuta mimi, wananchi tukiiachia serikali
pekeyake umeme huu hatuwezi kuupata mapema lakini tukichangia nguvu zetu umeme
utawaka june mwaka huu yaani miezi miwili tu ijayo kiongozi anayekataa kuleta
maendeleo ni mbya sana angekuwepo hapa ningemchapa fimbo mbele yenu bahati yake
amekimbia.’’ alisisitiza Filikunjombe
Akiongea kwa hasira mmoja wa wananchi wa
kijiji cha Luilo Bi.Stera Haule alidhibitisha kuwa Mh.Kongo alikuwa akipiga
kampeni ya kuwahamasishi wananchi kutokushiriki katika kazi hiyo ya kimaendeleo
baada ya Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe kufanya mikutano na
wananchi na kuwahimiza kushirikiana na wataalamu wa umeme katika kuchimba
mashimo hayo ili kuharakisha mradi huo kutekelezwa kwa muda mfupi.
Bi.Stera alisema wananchi wanachohitaji
ni maendeleo na si siasa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri nishati hiyo
ya umeme itapatikana lini lakini baadhi ya viongozi ambao ni tegemeo kwa chama
cha mapinduzi wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa ilani ya chama hicho ambayo
inataka kuleta maendeleo wa wananchi na Taifa kwa unjumla kwa muda mfupi.
Akitoa taarifa kwa mbunge Afisa mtendaji
wa kata ya Luilo Daniel Henjewele kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
kijiji cha Lifua alisema kuwa yeye alimtaarifu diwani wake kuhusu ziara ya
mbunge lakini akamjibu kuwa anakwenda kuhudhuri kikao cha kamati ya mipango na
fedha wilayani kwa sababu kina posho na yeye hana fedha ya kula.
‘’ mimi nilimtaarifu diwani wangu kuhusu
ziara ya mheshimiwa mbunge lakini alisema hawezi kuhudhuria ziara ya mbunge kwa
sababu anakwenda kwenye kikao cha kamati ya fedha na hana fedha ya kula, mimi
sina kosa na wala sizuii maendeleo na mimi ni mtendaji ila anayezuia
anafahamika hayupo hapa’’ alisema Henjewele
Kwa upande wake mkurugenzi wa uendeshaji
katika kampuni ya power magic electrica contractor Aron makulu alisema kama
wananchi watasubiri serikali na mkandarasi kufanyakazi zote mradi huu
unawezakukamilika hapo mwakani lakini kama mpango wa mh, Filikunjombe
utawezekana na wananchi kujitokeza kwa wingi mradi unaweza kukamilika baada ya
miezi miwili tu.
Akizungumza kwa njia ya simu matei kongo
alikana kuhamasisha wananchi kukataa kushiriki maendeleo kwa kusafisha njia na
kuchimba mashimo kwa ajili ya nguzo lakini akakiri kuwaambia wananchi kuwa kazi
ya kuleta maendeleo ni jukumu la
serikali na siyo wananchi kwa hiyo wananchi wanapaswa kulipwa. Hata hivyo
wananchi wamepuuza kauli za diwani huyo na kuamua kwa kauli moja kushirikiana
na mbunge wao kujiletea maendeleo.
Katika mradi huo vijiji 14 vya tarafa ya
masasi vitanufaika ikiwemo Ngalawale, Kimelembe, Mkomang’ombe,Kipangala,
Luilo,Lifua, Lihagule,Kingole,Igalu,Mbongo, Nsungu, Ilela,Ngelenge na Kipingu
kama wananchi watajitokeza kwa wingi kupitia nguvukazi zao utakamilika ndani ya
kipindi cha miezi miwili. @habari ludewa blog
No comments:
Post a Comment